• HABARI MPYA

  Sunday, January 15, 2017

  BLAGNON WA SIMBA ATIMKIA UARABUNI

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI wa Simba, Frederick Blagnon ameondoka Dar es Salaam leo kwenda Oman kupitia kwao Ivory Coast kwa ajili ya mipango ya kujiunga na Fanja ya nchini humo.
  Bin Zubeiry Sports - Online inafahamu kwamba Blagnon anakwenda kwao, Ivory Coast kushughulikia visa haraka ili aende Oman kufanyiwa vipimo vya afya tayari kujiunga na Fanja.
  Na Katibu wa Simba, Patrick Kahemele akathibitisha alipoulizwa; “Ni kweli kaondoka kwa ajili ya mipango ya kwenda kujiunga na timu moja ya Oman, bado hatujaijua.
  Frederick Blagnon anakwenda Oman kwa ajili ya mipango ya kujiunga na Fanja  

  Atapitia kwao, baadaye atakwenda Ivory Coast,”amesema.
  Blagnon aliyekuwa analipwa zaidi Simba, dola za Kimarekani 3,000 (zaidi ya Sh. Milioni 6) kwa mwezi alijiunga na Simba SC Julai mwaka jana kutoka African Sports ya kwao kwa dau la Sh. Milioni 100, ambazo zilitolewa na mfanyabiashara Mohamed Dewji anayetaka kununua hisa kwenye klabu hiyo.
  Hata hivyo, pamoja na kusajiliwa kwa dau kubwa na kulipwa mshahara mkubwa, mchezaji huyo ameshindwa kung’ara kwenye kikosi cha timu hiyo hata Simba imeridhia mpango wa kumuuza Oman.
  Na hiyo inafuatia timu kuimarisha safu yake ya ushambuliaji katika dirisha dogo Desemba kwa kumsajili mchezaji Mtanzania, Juma Luizio mwenye uzoefu wa mashindano makubwa kutoka Zesco United ya Zambia.
  Pamoja na Luizio aliyekwenda Zambia akitokea Mtibwa Sugar ya Morogoro, Simba SC imemsajili kiungo mshambuliaji chipukizi, Pastory Athanas kutoka Stand United ya Shinyanga, ambaye naye ameanza vizuri.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BLAGNON WA SIMBA ATIMKIA UARABUNI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top