• HABARI MPYA

  Saturday, January 07, 2017

  BEN POL AACHIA WIMBO MPYA MATATA SANA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MWANAMUZIKI wa muziki wa  kizazi kipya Benard Paul 'Ben Pol, ameachia wimbo mpya, unaitwa 'Phone, akimshirikisha mwanamuziki kutoka nchini Nigeria Mr. Eazi. 
  Akizungumza leo mjini Dar es Salaam, Pol alisema kuwa wimbo huo ameutengeneza katika studio ya  One love records, iliyopo jijini Dar es Salaam chini ya mtayarishaji Tiddy Hotter. 
  Pol alisema ujio wa wimbo huo ni moja ya mipango yake ya mwaka 2017 na ameanza kwa kutoa wimbo huo wa  'Phone'. 
  Ben Pol ameachia wimbo mpya, uitwao Phone ambao tayari umeanza kuchezwa kwenye vituo vya Redio na Televisheni mbalimbali nchini

  Alisema kuwa tayari wimbo huo umeanza kusikika kupitia vituo mbalimbali vya radio, huku ujio wa video yake ukiwa njiani. 
  "Wimbo wa Phone ni moja ya malengo yangu ya mwaka huu na ndiyo ujio wangu wa 2017, naomba wapenzi waupokee na kuusikiliza kila mtu ataelewa nini nimejipanga kupitia mwaka huu"alisema Pol. 
  Mwanamuziki huyo anayetamba na nyimbo mbalimbali ikiwemo pamoja na, Moyo Mashine, Maneno, Sofia, Pete, Maumivu, Samboira na ameshirikishwa kwenye wimbo wa Darasa unaotamba kwa sasa nchini unaitwa muziki. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BEN POL AACHIA WIMBO MPYA MATATA SANA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top