• HABARI MPYA

  Thursday, January 12, 2017

  ARSENAL YAWATIA PINGU WAFARANSA WAKE WATATU

  KLABU ya Arsenal imetangaza kuwaongezea mikataba wachezaji wake watatu Wafaransa, Olivier Giroud, Laurent Koscielny na Francis Coquelin, huku iki mbioni pia kuwaongezea mikataba na Mesut Ozil na Alexis Sanchez.
  Arsene Wenger amechangia kwa kiasi kikubwa klabu kufanikisha mpango wa kuwatia pingu wachezaji hao tegemeo kwa sasa The Gunners.
  Beki Koscielny, mwenye umri wa miaka 31, sasa anataka kumalizia soka yake London Kaskazini kwa kusiani mkataba wa miaka mitatu na nusu utakaomfanya adumu hadi mwaka 2020 akilipa Pauni 80,000 kwa wiki.
  The Gunners pia itaendelea kupata huduma za Giroud na Coquelin. Katika mkataba wa miaka miwili na nusu aliosaini, mshahara mpya wa Giroud ni Pauni 90,000 kwa wiki na sasa atadumu Emirates hadi mwaka 2019, wakati Coquelin amesaini miaka minne na nusu na sasa atakuwa akilipwa Pauni 75,000 kwa wiki. 

  Kutoka kushoto mbele ya kocha Arsene Wenger ni Francis Coquelin, Laurent Koscielny na Olivier Giroud ambao wote wamesaini mikataba mipya Arsenal  PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL YAWATIA PINGU WAFARANSA WAKE WATATU Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top