• HABARI MPYA

  Friday, December 16, 2016

  ZULU WA YANGA HATARINI KUWAKOSA JKT RUVU KESHO, WAGHANA WA SIMBA SAFI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIUNGO mpya wa Yanga, Justin Zulu kutoka Zambia yuko hatarini kuukosa mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya JKT Ruvu.
  Hiyo inafuatia Hati yake ya Uhamisho wake wa Kimataifa (ITC) kutotumwa hadi sasa na maana yake bila kibali hicho hawezi kucheza.
  Wakati ITC ya Zulu ikiwa haijafika, vibali vya wachezaji wawili wapya wa kigeni wa Simba kutoka Ghana, kipa Daniel Agyei na kiungo James Kotei wako huru kucheza Ligi Kuu kuanzia mzunguko wa pili unaoanza Jumamosi wiki hii.
  Kaimu Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jonas Kiwia aliiambia Bin Zubeiry Sports - Online jana kwamba tayari ITC za wawili hao zimetumwa na wako huru kucheza kuanzia Jumamosi. 
  Justin Zulu (kushoto) yuko hatarini kuukosa mchezo wa kesho wa dhidi ya JKT Ruvu kwa sababu ITC yake haijatumwa 

  “ITC za wachezaji wote wapya wa kigeni wa Simba zimetumwa na maana yake huru kucheza. Ila hiyo ya Zulu bado haijafika hadi sasa”alisema Kiwia.
  Ligi Kuu inatarajiwa kuanza kesho, Yanga ikianza na JKT Ruvu Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, wakati Simba itaanza na Ndanda FC mjini Mtwara Jumapili.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ZULU WA YANGA HATARINI KUWAKOSA JKT RUVU KESHO, WAGHANA WA SIMBA SAFI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top