• HABARI MPYA

    Saturday, December 17, 2016

    ZULU APANDISHWA JUKWAANI YANGA NA JKT RUVU HANA KIBALI CHA KUFANYA KAZI NCHINI

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KIUNGO mpya wa Yanga, Justin Zulu ameondolewa ghafla katika kikosi cha Yanga kinachocheza na JKT Ruvu jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kutokana na kutopata kibali cha kufanya kazi nchini.
    Mapema jana Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilionya mchezaji ambaye hatakuwa na kibaki cha kufanya kazi nchini kutoka Idara ya Uhamiaji hatacheza na Yanga inakuwa ya kwanza kukumbana na kibano hicho.
    Yanga inamenyana na JKT Ruvu kuanzia Saa 10:00 jioni ya leo katika mchezo wa kwanza wa mzunguko wa pili Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na Zulu hayumo kabisa.
    Awali, jina lake liliwekwa kwenye kikosi cha watakaoanzia benchi, lakini baadaye likaondolewa na kuwekwa jina la Said Juma ‘Makapu’.
    Justin Zulu hachezi leo kutokana na kutopata kibali cha kufanya kazi nchini

    Kikosi cha Yanga kinachoanza dhidi ya JKT Ruvu sasa ni; Deogratius Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Mwinyi Haji, Kelvin Yondani, Vincent Bossou, Thabani Kamusoko, Simoni Msuva, Haruna Niyonzima, Donald Ngoma, Amissi Tambwe na Deus Kaseke.
    Katike benchi baada ya kuondolewa Zulu wanabaki Ally Mustafa ‘Barthez’, Hassan Kessy, Vincent Andrew, Obrey Chirwa, Juma Mahadhi, Said Juma ‘Makapu’ na Geofrey Mwashiuya.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ZULU APANDISHWA JUKWAANI YANGA NA JKT RUVU HANA KIBALI CHA KUFANYA KAZI NCHINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top