• HABARI MPYA

    Wednesday, December 07, 2016

    YANGA MZIGONI JUMAMOSI NA JKU SHAMBA LA BIBI

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    YANGA SC itamenyana na JKU ya Zanzibar Jumamosi Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam katika mchezo wa kirafiki, ambao utakuwa wa kwanza tangu mabadiliko ya benchi la Ufundi mwezi uliopita.
    Novemba Yanga imeleta Maofisa wapya wawili wa benchi la Ufundi, Kocha Mkuu George Lwandamina na Msaidizi, Noel Mwandila wote Wazambia.
    Aliyekuwa Kocha Mkuu, Mholanzi Hans van der Pluijm anakuwa Mkurugenzi wa Ufundi wakati wasaidizi wake wote, Juma Mwambusi, Juma Pondamali kocha wa makipa, Meneja Hafidh Saleh, Daktari Edward Bavu, Mchua Misuli Jacob Onyango na Mtunza Vifaa, Mohammed Omar ‘Mpogolo’ wanaendelea kufanya kazi chini ya Wazambia.
    Wachezaji wa Yanga wakijifua Uwanja wa Gymkhana, Dar es Salaam leo
    Wachezaji wa Yanga wakijifua Uwanja wa Gymkhana, Dar es Salaam leo
    Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma yuko fiti 

    Na baada ya mabadiliko hayo, Yanga itacheza mechi yake ya kwanza Jumamosi dhidi ya wakali wa Visiwani, JKU ambao utakuwa maalum kuiandaa timu kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
    Siku hiyo mashabiki wa Yanga watapata fursa ya kumuona kwa mara ya kwanza kiungo Mzambia, Justine Zulu aliyesajiliwa mapema mwezi huu. 
    Ligi Kuu inatarajiwa kuanza Desemba 17 na Yanga itafungua dimba na JKT Ruvu Stars, iliyofanya mababadiliko ya benchi la Ufundi pia, ikimleta kocha Bakari Shime.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA MZIGONI JUMAMOSI NA JKU SHAMBA LA BIBI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top