• HABARI MPYA

    Monday, December 05, 2016

    WANA SIMBA PUUZENI POROJO NA HEKAYA ZA HOVYO

    "NAAMKA asubuhi nikiwa bukheri wa afya, huku nikiwa nimepata mapumziko mazuri ya weekend, sanjari na kupata fursa ya kuwajulia hali ndugu zangu wa kariakoo na kuhudhuria mikutano ya kidini na maulid jpili hii kule Msaasani kwa swahiba wangu Zingizi. 
    kama ilivyo ada baada ya kufanya mazoezi kdogo na kuunyosha mwili napitia taarifa za magazeti ya leo kwenye television, napatwa butwaa tena kuona porojo zimetamalaki ktk baadhi ya magazeti, yapo yalioandika kuhusu Daniel Aggey kipa wetu mpya, eti kaugomea uongozi kuhusu usajili, mengine kuhusu Jonas Mkude na Ibrahim Hajib. Hawa imeripotiwa eti wamesajili Yanga na mengine yapo yaliyozungumzia Mohammed 'Mo' Dewji kajitoa Simba.
    Kiungo wa Simba, Jonas Mkude (kushoto) katika mechi dhidi ya African Lyon mwezi uliopita
    Kwa kadri ninavyofahamu ni wajibu wa mwandishi 'ku-balance' story upande wa pili baada ya kupata hiyo story huko alipoiokota.
    Lakini kinachoonekana hizi story znatungwa tu na baadhi ya waandishi ama kwa nia ya kuuza magazeti au kwa nia ya kutugombanisha na mashabiki wetu, na katika hili wapo wanaoamua kujitoa kimasomaso kwa kunipigia kutaka kubalane hizi porojo!!
    Vp kuhusu Hajib kwenda Yanga unasemaje? Na tunaona picha ya Mkude na Msuva mitandaoni, twaambiwa ndiyo anampeleka Yanga. Je, Simba ina kauli gani? 
    Huwa naumia sana kuulizwa maswali ya aina hii. Yaani mtu anatunga story kisha mimi ndiyo nibalance, huku ni kunikosea kulikopitiliza. Na ni kuivunjia heshma klabu kulikovuka mipaka!!
    Niwahakikishie wachezaji wote hao ni mali ya Simba na taarifa zote za kwenda Yanga au kugoma kusajili ni uongo *'mkuu'*unaofaa kupuuzwa kwa kiwango cha kupuuza uvumi wa mtu kugeuka chatu... 
    Na hili la MO kujitoa ni aina ya jambo la hovyo kabisa, ninaongea na MO mara kwa mara, sijui hawa waandishi wanaitafuta nini Simba? Halafu ukiisoma story, eti ni habari za ndani. Ndani wapi? Uvunguni! 
    Nitoe wito kwa wana Simba tena na tena, taarifa za usajili au zozote zile nitatoa mimi au viongozi wa klabu, siyo mwingine yeyote.
    Zipuuzeni taarifa za kutengenezwa. Tukiwa na jambo tutawajulisha rasmi. Pia niwasihi waandishi wenzangu, hasa wale watungao story, wanapoteza heshima yao na wanainajisi taaluma hii muhimu sana.
    Kwangu mimi binafsi nitaendelea kushirikiana na wao kwa kila hali, ili kwa pamoja tubaki na weledi na maadili ya kazi hii inayobeba muhimili mkuu wa nne wa nchi,"
    (Makala hii imeandikwa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba, Hajji Sunday Manara, maalum kutolewa ufafanuzi masuala mbalimbali ya klabu yanayodaiwa kupotoshwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WANA SIMBA PUUZENI POROJO NA HEKAYA ZA HOVYO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top