• HABARI MPYA

  Saturday, December 17, 2016

  REFA WA ZAMBIA KUCHEZESHA FAINALI KOMBE LA DUNIA

  REFA wa kimataifa wa Zambia, Janny Sikazwe (pichani juu) atachezesha fainali ya Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA kati ya Real Madrid na Kashima Antlers.
  Janny Sikazwe atapuliza kipyenga hicho kesho kwenye mchezo huo baina ya Real Madrid na Kashima Antlers Uwanja wa Kimataifa wa Yokohama kuanzia Saa 5:30 asubuhi. 
  Hiyo itakuwa mara ya kwanza kwa refa wa Zambia kuchezesha mechi ya Real Madrid. 
  Katika mashindano haya, awali alichezesha mechi kati ya Kashima Antlers na Auckland City, iliyomalizika kwa timu ya Japan kushinda 2-1.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: REFA WA ZAMBIA KUCHEZESHA FAINALI KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top