• HABARI MPYA

  Thursday, December 15, 2016

  SAMATTA MAMBO SAFI UBELGIJI, GENK YAENDA NUSU FAINALI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta jana alicheza kwa dakika 105 akiisaidia timu yake KRC Genk kuingia Nusu Fainali ya Kombe la Ubelgiji baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Sporting Charleroi Uwanja wa Pays de Charleroi mjini Charleroi.
  Samatta hakufunga bao juzi na baada ya kupigana uwanjani kwa dakika 105 alitolewa ili kumpisha kiungo Tino-Sven Susic kutoka Bosnia na Herzegovina, wakati timu huo timu hizo zikiwa zimefungana bao 1-1 na ndipo Genk ilipokwenda kupata ushindi wake. 
  Shujaa wa Genk jana alikuwa Nikolaos Karelis aliyefunga mabao yote matatu dakika za 69, 94 na 116, wakati bao pekee la ya Sporting Charleroi lilifungwa na Steeven Willems dakika ya 83. 
  Mbwana Samatta jana alicheza kwa dakika 105 akiisaidia timu yake KRC Genk kuingia Nusu Fainali ya Kombe la Ubelgiji  

  Huo ulikuwa mchezo wa 34 jumla kwa Samatta kucheza Genk tangu awasili Januari mwaka huu kutoka TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC),18 msimu uliopita na 16 msimu huu. 
  Kati ya hizo, ni mechi 16 tu alianza, 10 msimu uliopita na sita msimu huu, 18 alitokea bench inane msimu uliopita na 10 msimu huu, wakati nane hakumaliza baada ya kutolewa, sita msimu uliopita na mbili msimu huu huku akiwa amefunga jumla ya mabao nane, matatu msimu huu na matano msimu uliopita.
  Kikosi cha KRC Genk kilikuwa; Bizot, Walsh, Colley, Brabec, Castagne, Ndidi, Pozuelo, Trossard, Bailey/Buffalo dk77, Samatta/Susic dk105 na Karelis/Dewaest dk119.
  Charleroi: Mandanda, Zajkov, Tainmont/Bedia dk81, Pollet, Diandy, Mata, Bakar/Benavente dk69, Willems, Marcq, N'Ganga na Fall/Baby dk81.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA MAMBO SAFI UBELGIJI, GENK YAENDA NUSU FAINALI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top