• HABARI MPYA

    Monday, December 05, 2016

    SAMATTA ATOKEA BENCHI NA KUSHINDWA KUINUSURU GENK NA KIPIGO

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta usiku wa jana ametokea benchi na kushindwa kuinusuru timu yake, KRC Genk kulala 2-1 nyumbani mbele ya Lokeren Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk.
    Katika mchezo huo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji, Samatta aliingia dakika ya 81 kwenda kuchukua nafasi ya mshambuliaji mkongwe, Thomas Buffel.
    Kocha wa Genk, Peter Maes atajilaumu mwenyewe kwa kuwadharau Lokeren na kuwaanzishia kikosi dhaifu kabla ya kuwainua baadhi ya wachezaji wake tegemeo kipindi cha pili, wakati wapinzani wamekwishaumudu mchezo. 
    Ikumbukwe mchezo uliopita, Samatta alifunga mabao mawili katika ushindi wa 3-1 dhidi ya wenyeji, Waasland-Beveren kwenye mchezo wa Kombe la Ubelgiji Uwanja wa Freethiel-Stadion mjini Beveren-Waas.
    Samatta (kushoto) alifunga mbao mawili katika ushindi wa 3-1 dhidi ya wenyeji, Waasland-Beveren kwenye mchezo uliopita

    Jana Samatta amecheza mechi ya 37 tangu ajiunge na Genk Januari mwaka huu kutoka TP Mazembe ya DRC, 18 msimu uliopita na 17 msimu huu, akifunga mabao 10, matano msimu huu na matano msimu uliopita.
    Katika mechi hizo, ni 19 tu ndiyo alianza, 10 msimu uliopita na saba msimu huu, wakati 17 alitokea benchi nane msimu uliopita na 14 msimu huu – na mechi 10 hakumaliza akitolewa, sita msimu uliopita na nne msimu huu.
    Kikosi cha KRC Genk kilikuwa: Bizot, Walsh, Colley, Dewaest, Castagne, Ndidi, Heynen/Susic dk81, Pozuelo, Trossard, Buffalo/Samatta dk81 na Karelis.
    Lokeren: Copa, Maric, Skulason, Overmeire, De Sutter/Ninaj dk84, Galitsios, Terki, Ingason, Huppert/Miric dk70, Ticinovic/Rocketman Stra dk59 na Bolbat.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SAMATTA ATOKEA BENCHI NA KUSHINDWA KUINUSURU GENK NA KIPIGO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top