• HABARI MPYA

  Thursday, December 01, 2016

  PHIRI SASA ROHO KWATU MBEYA CITY

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KOCHA wa Mbeya City, Mmalawi Kinnah Phiri amesema kwamba kwa sasa roho yake iko kwatu katika klabu hiyo kufuatia wachezaji kuanza kumuelewa na kuelewana pia.
  “Niko sawa kwa sasa, sina malalamiko tena. Nafsi yangu iko vizuri, baada ya timu kuanza kukaa vizuri. Sasa nafikiria namna ya kujipanga kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu,”alisema.
  Phiri alisema kwamba anatarajiwa kurejea Mbeya leo kutoka mapumzikoni kwa Malawi, kufuatia kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu.
  Kinnah Phiri amesema kwamba kwa sasa roho yake iko kwatu katika klabu hiyo kufuatia wachezaji kuanza kumuelewa na kuelewana pia

  Na alisema kwamba anatarajia uongozi utakuwa umefanyia kazi mapendekezo yake ya usajili wa wachezaji wapya wa kuongeza nguvu katika mzunguko wa pili.
  “Nitakuwa ⁠⁠⁠Mbeya Alhamisi kuanza kuiandaa kwa mzunguko wa pili. Mengi zaidi tutafahamishana baada ya kufika huko na kuwasiliana na uongozi,”alisema.
  Mbeya City ilimaliza nafasi ya nane mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa pointi zake 19 za mechi 15, sawa na mahasimu wao wa Jiji la Mbeya, Prisons waliomaliza nafasi ya saba.
  Wakati huo huo: Mtunza vifaa wa Mbeya City, Rashid Kasiga amesema kwamba bado kuna tatizo kubwa la ubora wa vifaa vinavyotolewa kwa timu zinazoshiriki Ligi Kuu.
  “Kuna malalamiko makubwa juu ya ubora wa vifaa, wachezaji wamekuwa wakilalamika kuhusu mipira, jezi na vifaa vingine kuwa haviko kwenye viwango sawa jambo ambalo limekuwa likiwakosesha ufanisi kwenye kazi yao, tunatumia mipira ambayo haina kiwango kizuri huwezi kupiga shuti likahesabika, jezi mara mbili tu zimechanika hakika wadhamini wanapaswa kulitizama hili,”alisema.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PHIRI SASA ROHO KWATU MBEYA CITY Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top