• HABARI MPYA

  Sunday, December 18, 2016

  OMOG AWAVAA MDANDA KIFUA MBELE; ASEMA USHINDI LAZIMA LEO NANGNWANDA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KOCHA Mcameroon wa Simba SC, Joseph Omog amesema ana matumaini ya kuanza vizuri mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara leo.
  Simba watakuwa wageni wa Ndanda FC leo jioni Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara na baada ya mazoezi ya jana kwenye Uwanja huo, Omog alisema kwamba wana matumaini ya ushindi.
  “Ni matumaini yangu tutashinda kesho, baada ya mazoezi hapa nimeona timu yangu iko vizuri kabisa na vijana wako tayari kuendeleza kazi nzuri waliyoianza mzunguko wa kwanza,”alisema Omog, kocha wa zamani wa Azam.
  Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba, Hajji Sunday Manara alisema wachezaji wao wote wapya kutoka Ghana, kipa Daniel Agyei na kiungo James Kotei wako huru kucheza leo baada ya kukamilisha taratibu zote.
  “Napenda kuchukua nafasi kuwataka wapenzi wa Simba na Mtwara na maeneo jirani wajitokeze kwa wingi kuipa sapoti timu yao leo. Na hakuna shaka wachezaji wetu wote wa Ghana wao huru kucheza baada ya kukamilishiwa taratibu zote,”alisema.
  Manara alisema taratibu hizo ni pamoja na kupatiwa Hati za Uhamisho wa Kimataifa (ITC) na vibali vya kufanya kazi nchini kutoka Idara ya Uhamiaji.
  Ikumbukwe SImba SC ilimaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ikiwa inaongoza kwa pointi zake 35 za mechi 15, ikiwazidi kwa pointi mbili mabingwa watetezi, Yanga.
  Lakini baada ya Yanga kushinda 3-0 jana dhidi ya JKT Ruvu wamepanda kileleni kwa kufikisha pointi 36, hivyo Simba wanahitaji ushindi leo ili kurejea tena kileleni. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: OMOG AWAVAA MDANDA KIFUA MBELE; ASEMA USHINDI LAZIMA LEO NANGNWANDA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top