• HABARI MPYA

  Thursday, December 15, 2016

  NGASSA ATUA MBEYA KUKAMILISHA USAJILI WAKE CITY

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SAALAAM
  TIMU ya Mbeya City iko mbioni kukamilisha usajili wa mchezaji nyota wa kimataifa wa Tanzania, Mrisho Khalfan Ngassa kutoka klabu ya Fanja ya Oman.
  Ngassa aliwasili Mbeya jana kwa taratibu za mwisho za usajili wake katika timu hiyo baada ya kuachana na Fanja, aliyodumu nayo kiwa mwezi mmoja na ushei.
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports - Online leo, Ngassa amesema kwamba yuko mjini Mbeya kwa taratibu za mwisho za usajili wake ambazo hadi mchana wa jana zilikuwa hazijakamilika. 
  “Nafikiri ndoto ya muda mrefu ya Mbeya City kummiliki Mrisho Ngassa inakaribia kutimia. Nipo hapa kwa mazungumzo ya mwisho na kukamilisha taratibu za usajili, baada ya kufikia makubaliano matika mazungumzo ya awali Dar e Salaam,”amesema.
  Mrisho Ngassa amewasili Mbeya jana kwa taratibu za mwisho za usajili wake katika timu hiyo baada ya kuachana Fanja 
  Amesema atafurahi taratibu hizo zikikamilika, kwani atajiunga na Kocha Mmalawi, Kinnah Phiri ambaye awali alifanya naye kazi Afrika Kusini katika klabu ya Free State Stars ya Bethlehem.
  Ngassa ambaye amechagua kwenda Mbeya City badala ya klabu nyigine mbili ambazo zilimtaka pia nchini, amesema atafurahi kucheza Ligi ya Tanzania iliyompatia umaarufu na kumkuza kisoka.
  Ngassa alijiunga na Fanja Septemba 21 kwa mkataba wa miaka miwili akitokea ya Free State Stars, alikoondokaAgosti mwaka huu baada ya kuomba mwenyewe kuvunja Mkataba kama ilivyokuww Fanja.
  Ngassa alijiunga na Free State Stars Mei mwaka jana akisajiliwa na kocha Mmalawi, Kinnah Phiri kwa mkataba wa miaka minne.
  Hata hivyo, kocha aliyemsajili baba huyo wa Farida (9) na Faria (7) alifukuzwa baada ya miezi miwili tu na sasa tayari yuko Mbeya City ya Tanzania.
  Katika kipindi cha mwaka mmoja wa kuwa Free State, Ngassa alifanya kazi na makocha wanne akiwemo huyu wa sasa, Mfaransa Denis Lavagne aliyeanza kazi Juni mwaka huu.
  Wengine ni Mjerumani Ernst Middendorp aliyefanya kazi kati ya Septemba na Desemba 2015, Mtaliano Giovanni Solinas aliyefanya kazi kati ya Desemba na Mei 2016.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NGASSA ATUA MBEYA KUKAMILISHA USAJILI WAKE CITY Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top