• HABARI MPYA

    Sunday, December 04, 2016

    MWANAFUNZI WA MWANZA SECO AFARIKI BAADA YA KUIFUNGIA MBAO BUKOBA

    MSHAMBULIAJI wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Mbao FC ya Mwanza, Ismail Mrisho Khalfan amefariki dunia leo mjini Bukoba baada ya kuanguka uwanjani.
    Mchezaji huyo alianguka Uwanja wa Kaitaba, Bukoba dakika chache baada ya kuifungia bao timu yae katika ushindi wa 2-0 kufuatia kugongana na mchezaji wa Mwadui FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vijana Tanzania Bara.
    Baada ya kuanguka alipatiwa huduma ya kwanza na kuonekana hali yake si ya kawaida, hivyo kukimbizwa hospitali ya mkoa wa Kagera kwa matibabu zaidi, ambako umauti ulimfika.
    Mchezaji huyo amefariki akiwa ana umri wa miaka 19 na akiwa ametoka tu kufanya mtihani wa kidato cha Nne katika shule ya sekondari ya Mwanza, maarufu 'Mwanza Seco'.
    Ismail Mrisho Khalfan akishangilia baada ya kufunga bao la kwanza la Mbao 


    Ismail Mrisho Khalfan akipelekwa kwenye gari baada ya kuanguka uwanjani ili akimbizwe hospitali PICHA ZOTE NA FAUSTINE RUTTA
    Ismail Mrisho Khalfan akipatiwa huduma ya kwanza baada ya kuanguka uwanjani ili akimbizwe hospitali
    Gari lililombeba Ismail Mrisho Khalfan likielekea hospitali 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MWANAFUNZI WA MWANZA SECO AFARIKI BAADA YA KUIFUNGIA MBAO BUKOBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top