• HABARI MPYA

    Sunday, December 04, 2016

    KIKWETE AONGOZA MAZISHI YA MZIMBA LEO MSOGA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    RAIS mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete leo ameongoza mazishi ya kiongozi maarufu wa zamani wa klabu ya Yanga, Mzee Yussuf Mzimba kijijini Msoga, Chalinze mkoani Pwani.
    Mzimba alifariki dunia Alasiri ya juzi mjini Dar es Salaam katika hospitali ya Mwananyamala alipopelekwa kwa matibabu. Leo asubuhi mwili wake ulisaliwa Magomeni Kwa Bi Nyau, nyumbani kwa mwanawe mkubwa, Khalid kabla ya safari ya mazishi Msoga.
    Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na viongozi wengine mbalimbali walishiriki kikamilifu mazishi hayo kuanzia Magomeni hadi Msoga. 
    Marais; Rais mstaafu, Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akisalimiana na Rais wa TFF, Jamal Malinzi 



    Mzee maarufu wa Yanga, Ibrahim Akilimali akitoa hotuba fupi msibani Msoga


    Matayarisho ya mwisho ya kaburi la Mzee Mzimba
    Malinzi akizungumza na Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete (kulia)

    Mzimba amefariki dunia akiwa ana umri wa miaka 84 na enzi za ujana wake alikuwa Katibu Mwenezi wa Yanga miaka ya 1970 chini ya Mwenyekiti, Tarbu Mangara (marehemu pia).
    Ni sehemu ya viongozi waliofanikisha ziara maarufu za nje za klabu hiyo, Brazil mwaka 1973 na Romania mwaka 1978.
    Baada ya hapo, akaibuka kama mwanaharakati mwishoni mwa miaka ya 1990 kupinga timu hiyo kugeuzwa Kampuni, akiwa Mwenyekiti wa kikundi cha Yanga Asili.
    Alipambana na uongozi wa Yanga chini ya Mwenyekiti Tarimba Abbas na baadaye chini ya Francis Kifukwe kabla ya kupatanishwa na Mwenyekiti wa sasa, Yussuf Manji.
    Baada ya suluhu hiyo Mzimba akawa miongoni mwa Wazee wa heshima wa Yanga kabla ya kujiweka kando na shughuli za klabu mwaka 2013 kufuatia kuanza kusumbuliwa kiafya.  Mungu ampumzishe kwa amani Mzee Mzimba. Amin.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIKWETE AONGOZA MAZISHI YA MZIMBA LEO MSOGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top