• HABARI MPYA

    Tuesday, December 06, 2016

    JOSHUA KUZIPIGA NA KLITSCHKO APRILI 20 WEMBLEY

    BONDIA Wladimir Klitschko ametaja tarehe ya pambano lake kubwa la uzito wa juu na Muingereza, Anthony Joshua.
    Mkongwe huyo wa Ukraine, ambaye alikuwa bingwa asiyepingika kwa muongo mmoja, anatarajiwa kupanda ulingoni na mshindi wa Medali ya Dhahabu ya Olimpiki, Joshua Aprili 29 mwakani kwenye Uwanja wa Wembley, London.
    Hata hivyo, Uwanja wa Cardiff na viwanja vingine nchini Ujerumani navyo vinapewa nafasi ya kuhodhi pambano hilo.
    Pamoja na hayo taratibu za kusaini mikataba bado hazijakamilishwa.
    Klitshcko anatarajiwa kwenda kukamilisha taratibu za pambano hilo hivi karibuni katika safari yake ya Manchester kwenye pambano la AJ kutetea kwa mara ya pili taji lake la IBF dhidi ya Eric Molina Jumamosi.
    Anthony Joshua anatarajiwa kupambana na Wladimir Klitschko Uwanja wa Wembley, London Aprili 29, mwaka huu PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: JOSHUA KUZIPIGA NA KLITSCHKO APRILI 20 WEMBLEY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top