• HABARI MPYA

    Friday, December 16, 2016

    COWBELL WADHAMINI WA RUVU SHOOTING LIGI KUU

    Na Mwandishi Wetu, MLANDIZI
    KAMPUNI ya Hawaii Product Suppliers Limited leo imeingia mkataba mfupi wa udhamini na klabu ya Ruvu Shooting ya Pwani.
    Katika hafla fupi ya utiwaji saini mkataba huo iliyofanyika makao makuu ya timu hiyo Mlandizi, mkoani Pwani, Hawaii imeingia na mkataba na Ruvu Shooting inayomilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kupitia maziwa ya Cow Bell.
    Mhasibu wa kampuni ya Hawaii, Said Ali Khamis alisema jana kwamba mkataba huo wenye thamani ya Sh. Milioni 25 ni wa miezi sita kumalizia Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2016/2017 na unaweza kuongezwa iwapo Ruvu itabaki Ligi Kuu.
    Mhasibu wa kampuni ya Hawaii Products Suppliers Limited, Said Khamis (kushoto), akimkabidhi jezi yenye nembo ya maziwa ya Cowbell Mwenyekiti wa Ruvu Shooting, Luteni Kanali Charles Mbuge baada ya kusaini mkataba huo
    Mhasibu wa kampuni ya Hawaii Products Suppliers Limited, Said Khamis (kushoto), akimkabidhi jezi yenye nembo ya maziwa ya Cowbell Mwenyekiti wa Ruvu Shooting, Luteni Kanali Charles Mbuge baada ya kusaini mkataba huo

    “Tumeamua kuidhamini Ruvu Shooting baada ya kuvutiwa na kiwango kizuri cha ushindani cha mchezo walichoonyesha katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu na tunawatakia kila la heri katika mzunguko wa pili ili waiwakilishe vyema bidhaa yetu,”alisema mwakilishi huyo wa Hawaii.  
    Khamis alisema katika fedha hizo, Sh. Milioni 15 Ruvu Shooting wamepewa taslimu na Milioni 10 watapewa vifaa mbalimbali vya michezo.
    Akizungumza baada ya kusaini Mkataba huo, Mwenyekiti wa Ruvu Shooting, Kanali Charles Mbuge alisema kwamba wanashukuru kwa udhamini huo na wanaamini utakuwa ni chachu ya wao kufanya vizuri katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu.
    Katika hatua nyingine, Ruvu Shooting imesajili mchezaji mmoja tu kwenye dirisha dogo, ambaye ni Ismail Mohammed Mgunda aliyechezea Coastal Union msimu uliopita.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: COWBELL WADHAMINI WA RUVU SHOOTING LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top