• HABARI MPYA

  Friday, December 02, 2016

  CAMACHO KOCHA MPYA WA GABON, WENYEJI WA AFCON 2017

  KOCHA wa zamani wa Real Madrid, Jose Antonio Camacho ameteuliwa kuwa kocha wa wenyeji wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2017, Gabon kuelekea michuano hiyo inayoanza Januari 14 hadi Februari 5.
  Babu huyo wa umri wa miaka 61 sasa, ambaye atafuata nyayo za kocha Mreno, Jorge Costa, amekuwa mjini Libreville tangu Jumamosi kwa mazungumzo na Rais wa Shirikisho la Soka Gabon (Fegafoot), Alain Pierre Mounguengui.
  Jukumu la kwanza la Camacho ni kuwaandaa Les Pantheres zikiwa zimebaki wiki sita kabla ya kuanza Afcon na lengo la kwanza ni kuifikisha timu hiyo Robo Fainali kutoka hatua ya makundi.
  Jose Antonio Camacho ameteuliwa kuwa kocha wa wenyeji wa Afcon ya 2017, Gabon

  Gabon imepangwa Kundi A pamoja na Cameroon, Burkina Faso na Guinea Bissau wanaoshiriki kwa mara ya kwanza.
  Les Pantheres wataanza kampeni ya kuwania taji lao la kwanza la Afcon 2017 kwa kumenyana na Guinea Bissau Januari 14 Uwanja wa de l’Amitie mjini Libreville kabla ya kuivaa Burkina Faso Januari 18 kwenye Uwanja huo huo na kisha kumaliza na Cameroon katika mechi ya mwisho ya Kundi A itakayokutanisha wapinzani wa Afrika ya Kati.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CAMACHO KOCHA MPYA WA GABON, WENYEJI WA AFCON 2017 Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top