• HABARI MPYA

    Sunday, December 04, 2016

    BOSSOU 'ATIA TIMU' LEO JANGWANI

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    BEKI Mtogo wa Yanga, Vincent Bossou anatarajiwa kurejea nchini leo kujiunga na wenzake kwa maandalizi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
    Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online leo kwamba Bossou atakuwa mazoezini kesho baada ya kuwasili leo.
    “Amepiga simu amesema anakuja leo. Na kama akifika leo maana yake kesho atakuwa mazoezini,”amesema Hafidh.
    Bossou akiwasili atafanya idadi ya wachezaji walioripoti mazoezini Yanga kufika 24 tangu kocha mpya, Mzambia George Lwandamina aanze kazi wiki Jumatatu wiki hii.
    Kiungo chipukizi, Yussuf Mhilu aliyepandishwa msimu huu kutoka timu ya vijana, ambaye yupo na kikosi cha U-20 Bukoba mkoani Kagera kwenye Ligi Kuu ya Vijana ndiye atakayekuwa anasubiriwa kukamilisha idadi ya wachezaji wa timu hiyo.
    Wengine ni makipa Ally Mustafa ‘Barthez’, Deo Munishi ‘Dida’, Benno Kakolanya, mabeki Hassan Kessy, Oscar Joshua, Mwinyi Hajji Mngwali, Kevin Yondan, Pato Ngonyani, Juma Abdul, Andrew Vincent ‘Dante’ na Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’.
    Wengine ni viungo Justine Zulu, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Deus Kaseke, Mkongo Mbuyu Twite, Geofrey Mwashiuya, Juma Mahadhi, Said Juma, Mzimbabwe Thabani Kamusoko na washambuliaji Mrundi Amissi Tambwe, Mzimbabwe Donalde Ngoma, Malimi Busungu na Matheo Anthony.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BOSSOU 'ATIA TIMU' LEO JANGWANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top