• HABARI MPYA

    Tuesday, December 06, 2016

    BOSSOU AANZA KUJIFUA YANGA, AWAONYA WAANDISHI WAACHE KUMPAKAZIA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    BEKI wa Yanga, Vincent Bossou raia wa Togo mwenye asili ya Ivory Coast, jana alianza mazoezi na wenzake Uwanja wa Gymkhana, Dar es Salaam kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
    Bossou aliwasili Dar es Salaam juzi jioni kutoka Togo ambako alichelewa kwa majukumu ya timu yake ya taifa iliyokuwa kwenye maandalizi ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika.
    Na baada ya kuwasili, Bossou alisema kwamba amesikitishwa na taarifa za kwenye vyombo vya habari wakati akiwa Togo kwamba anataka kuiacha klabu hiyo.
    Vincent Bossou (kulia) jana alianza mazoezi Yanga baada ya kurejea juzi kutoka kwao, Togo  

    “Kwa kweli sipendi tabia ya vyombo vya habari Tanzania kuandika habari za uongo kuhusu mimi. Kama hawakuweza kunipata, kwa nini wasisubiri nirudi wakaniuliza kuliko kwenda kuandika au kutangaza uongo?”alihoji.
    kulikuwa kuna habari kwamba Bossou hatarejea, kwa sababu anafanya mpango wa kujiunga na klabu moja ya Vietnam jambo ambalo mchezaji mwenyewe amekanusha jana.
    Yanga inaendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Gymkhana kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara unaotarajiwa kuanza baadaye mwezi huu.
    Ikumbukwe mabingwa hao watetezi, walimaliza mzunguko wa kwanza katika nafasi ya pili kwa pointi zao 33 za mechi 15, wakizidiwa pointi mbili na vinara, Simba SC.     
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BOSSOU AANZA KUJIFUA YANGA, AWAONYA WAANDISHI WAACHE KUMPAKAZIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top