• HABARI MPYA

  Sunday, December 11, 2016

  AZAM NA MTIBWA SUGAR ZILIVYOTOSHANA NGUVU JANA CHAMAZI

  Winga wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Enock Atta Agyei, akijaribu kuwatoka wachezaji wa Mtibwa Sugar,  beki Salim Mbonde (pembeni) na winga Kelvin Friday wakati wa mchezo wa kirafiki uliofanyika usiku wa kuamkia leo ndani ya Uwanja wa Azam Complex, Chamazi. Timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2. Mabao ya Azam yalifungwa na Waghana Enock Atta Agyei kwa penalti na  Yahaya Mohammed, wakati ya Mtibwa yalifungwa na viungo Shaaban Nditi na Ibrahim Rajab ‘Jeba’
  Mshambuliaji wa Azam FC, Yahaya Mohammed, akijaribu kumtoka kiungo wa Mtibwa Sugar, Henry Joseph
  Nahodha wa Azam FC, John Bocco, akiambaa na mpira mbele ya wachezaji wa Mtibwa Sugar 
  Winga wa Azam FC, Samuel Afful, akimkimbiza beki wa Mtibwa Sugar, Hassan Mganga
  Winga wa Azam FC, Joseph Mahundi, akitafuta maarifa ya kumtoka beki wa Mtibwa Sugar, Ally Shomari.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM NA MTIBWA SUGAR ZILIVYOTOSHANA NGUVU JANA CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top