• HABARI MPYA

  Thursday, December 01, 2016

  AVEVA AWAITA FARAGHA WAKUU WA MATAWI SIMBA SC

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  RAIS wa klabu ya Simba, Evans Elieza Aveva Jumamosi atakutana na viongozi wa matawi ya klabu hiyo Dar es Salaam kujadiliana nao kuhusu Mkutano Mkuu wa klabu hiyo uliopangwa kufanyika Desemba 11 mwaka huu. 
  Msemaji wa Simba, Hajji Sunday Manara amesema leo kwamba kikao cha Rais Aveva na viongozi wa matawi kitaanza Saa 8:00 mchana kwenye ukumbi wa mikutano wa klabu, uliopo Mtaa wa Msimbazi, Dar es Salaam.
  Manara alisema kwamba kwa ujumla kikao hicho ni maandalizi ya Mkutano Mkuu maalum wa kujadili marekebisho ya Katiba uliopangwa kufanyika Desemba 11 Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oystrebay, Dar es Salaam. 
  Evans Aveva atakutana na viongozi wa matawi ya klabu hiyo Dar es Salaam Jumamosi

  Manara alisema pamoja na hayo, mkutano wa Rais na viongozi wa matawi, utajadili pia kwa kina maandalizi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, inayotarajiwa kuanza katikati ya mwezi huu. 
  Wakati huo huo: Kipa 
  Kipa Daniel Agyei kutoka klabu ya Medeama SC ya kwao, Ghana jana alianza mazungumzo na uongozi wa klabu hiyo juu ya kujiunga nayo.
  Kipa huyo aliyeng’ara katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika mwaka huu akiwa na Yanga SC, aliwasili Dar es Salaam juzi na moja kwa moja kupelekw kwenye hoteli moja ya nyota tatu Jijini kupumzika. 
  Na Simba itatakiwa kukata mchezaji mmoja wa kigeni ili kumsajili Agyei, kwani tayari ina wachezaji saba wanaokidhi kanuni za Ligi Kuu ambao ni kipa Vincent Angban kutoka Ivory Coast, mabeki Janvier Bokungu kutoka DRC, Juuko Murshid kutoka Uganda, Method Mwanjali kutoka Zimbabwe, kiungo Mussa Ndusha kutoka DRC na washambuliaji Frederick Blagnon kutoka Ivory Coast na Laudit Mavugo kutoka Burundi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AVEVA AWAITA FARAGHA WAKUU WA MATAWI SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top