• HABARI MPYA

  Tuesday, November 15, 2016

  YANGA YATAKA KUBEBA VIUNGO WAWILI MBEYA CITY

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  YANGA SC inafuatilia saini za wachezaji wawili wa safu ya kiungo ya Mbeya City, Kenny Ally na Raphael Daudi.
  Mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga SC wanataka kuimarisha kikosi chao kwa kuwasajili kiungo mkabaji na Nahodha wa MCC Kenny Ally na kiungo mchezeshaji Raphael Daud.
  Kwa staili yake mpya maarufu ya ‘mambo kimya kimya’, inadaiwa Yanga imefikia katika hatua nzuri kwenye mpango wa kuwasajili wawili hao waliopandishwa mwaka 2014 kutoka timu ya vijana ya Mbeya City.
  Kenny Ally akimtoka kiungo wa Simba, Mwinyi Kazimoto msimu uliopita
  Raphael Daudi (kushoto) akimfukuzia kiungo wa Yanga, Mbuyu Twite

  Lakini Mbeya City leo wametoa onyo kwa Yanga kupitia BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE; “Tumekuwa tukisikia taarifa za Yanga kuwataka hao wachezaji, lakini bado hawajazungumza na sisi. Ninachopenda tu kuwaambia Yanga ni kwamba, hao wachezaji wote wana mikataba na klabu,”amesema Dissmas Ten, Ofisa Habari wa Mbeya City.
  “Kila mmoja ana mkataba wa mwaka na nusu, kwa sababu ni mwaka jana tu wamesaini mikataba mipya. Sasa kama Yanga wanawataka, wafuate tu taratibu,”alisema Ten.
  Wawili hao wote ni matunda ya timu ya vijana ya Mbeya City na walipandishwa kikosi cha kwanza cha timu hiyo mwaka 2014, wakati huo timu hiyo ikiwa chini ya Juma Mwambusi, ambaye kwa sasa ni kocha Msaidizi wa Yanga.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YATAKA KUBEBA VIUNGO WAWILI MBEYA CITY Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top