• HABARI MPYA

  Monday, November 07, 2016

  YANGA NA RUVU SHOOTING UHURU, SIMBA NA PRISONS SOKOINE

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MECHI tatu za viporo za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara za raundi ya nane ya mzunguko wa kwanza, sasa zitafanyika Jumatano wiki hii.
  Mechi hizo ni kati ya Mwadui ya Shinyanga na Azam FC ya Dar es Salaam ambayo itachezwa Uwanja wa Mwadui, Shinyanga wakati Simba itasafiri hadi Mbeya kucheza na Prisons Uwanja wa Sokoine na mabingwa watetezi, Yanga SC watakuwa wenyeji wa Ruvu Shooting Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
  Awali pamoja na mechi hizo kuwekwa kwenye ratiba, lakini hazikuwa na tarehe huku ikielekezwa tarehe zitatajwa baadaye. 
  Yanga SC watakuwa wenyeji wa Ruvu Shooting Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam Jumatano

  Tayari Bodi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), imewasiliana na wahusika kuhusu mabadiliko hayo. Sababu ya kuvuta nyuma michezo hiyo ni kutoa nafasi ya maandalizi ya kambi ya timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayotarajiwa kusafiri Ijumaa wiki hii kwenda Harare Zimbabwe kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa unaotarajiwa kufanyika Novemba 13, maka huu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA NA RUVU SHOOTING UHURU, SIMBA NA PRISONS SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top