• HABARI MPYA

  Tuesday, November 08, 2016

  YANGA KUWAKOSA BOSSOU, TWITE MECHI NA RUVU SHOOTING KESHO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KOCHA wa Yanga, Mholanzi Hans van der Pluijm amesema atawakosa walinzi wake wawili tegemeo, Mkongo Mbuyu Twite na Mtogo Vincent Bossou katika mchezo wa kesho dhidi ya Ruvu Shooting.
  Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara itaendelea kesho kwa mechi tatu na mabingwa watetezi, Yanga SC watakuwa wenyeji wa Ruvu Shooting Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Simba watakuwa wageni wa Prisons Mbeya na Azam FC wataifuata Mwadui huko Shinyanga.
  Mbuyu Twite atakosekana kesho Yanga ikimenyana na Ruvu Shooting kwa sababu atakuwa anatumikia adhabu ya kadi

  Kuelekea mchezo huo, kocha Mholanzi Hans van der Pluijm amesema kwamba anasikitika atawakosa beki anayeweza kucheza kama kiungo pia, Twite na beki wa Kati Bossou.
  Pluijm amesema kwamba Twite atakuwa anatumikia adhabu ya kadi, wakati Bossou amerejea kwao kuichezea timu yake ya taifa, Togo katika mechi za kimataifa zinazoanza katikati ya wiki hadi mwishoni mwa wiki  
  “Tunachezaji na Ruvu Shooting katika mchezo mwingine wa lazima kushinda. Tutawakosa majeruhi Juma Abdul, Mbuyu Twitte ana kadi na Vincent Bossou amekwenda timu ya taifa ya Togo,”amesema Pluijm.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA KUWAKOSA BOSSOU, TWITE MECHI NA RUVU SHOOTING KESHO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top