• HABARI MPYA

    Saturday, November 19, 2016

    YAHYA HAMAD KAIMU MWENYEKITI KAMATI YA SAA 72 YA TFF

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    RAIS Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemteua Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Yahya Hamad kukaimu nafasi ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uendeshaji Ligi (Kamati ya Saa 72) ili kushughulia masuala yote ya mechi zilizochezwa tangu mwanzoni mwa Novemba, 2016 baada ya kifo cha Sheikh Muhammad.
    "Tunachukua nafasi hii kutoa wito kwa klabu kumpa ushirikiano Hamad katika majukumu yake mapya akiongoza kamati hiyo,"imesema taarifa ya TFF jana.
    Wajumbe wa Kamati hiyo ni Baruan Muhuza (Azam Tv), Boniface Wambura (Mtendaji Mkuu Bodi ya Ligi), Jonas Kiwia (Kaimu Mkurugenzi wa Mashindano TFF), Philemon Ntahilaja (Mdau wa Mpira wa Miguu), Charles Ndagala (Katibu Kamati ya Waamuzi ya TFF), Kanali Mstaafu wa JWTZ, Isaron Chacha na Steven Mnguto ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya ligi. 
    TFF imesema inawashukuru wanafamilia wa soka kwa salamu mbalimbali za rambirambi kutokana na msiba wa Mwenyekiti wa Azam FC na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu, Sheikh Said Muhammad aliyefariki dunia Novemba 7, 2016 katika Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam.
    Marehemu Sheikh Said Muhammad alikuwa hazina katika mpira wa miguu nchini kutokana na uwezo wake mkubwa wa kutoa mchango ya mawazo na miongozo katika Kamati ya Utendaji ya TFF. 
    Itakumbukwa kwamba Sheikh Muhammad aliongoza Klabu ya Azam kwa mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kubeba ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na Kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kagame Cup) kwa mara ya kwanza tangu klabu hiyo ianzishwe.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YAHYA HAMAD KAIMU MWENYEKITI KAMATI YA SAA 72 YA TFF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top