• HABARI MPYA

  Saturday, November 19, 2016

  WENGER NA MOURINHO KAZI IPO LEO MAN U NA ARSENAL OLD TRAFFORD

  MANCHESTR, England
  LIGI Kuu ya England inarejea leo baada ya mapumziko ya wiki moja kupisha mechi za kufuzu Kombe la Dunia 2018 Urusi- na gumzo kubwa ni mchezo baina ya Arsenal na Manchester United kuanzia Saa 9:30 Alasiri.
  Kocha Arsene Wenger wa Arsenal leo atakuwa anawania kuizidi kwa pointi tisa timu ya Jose Mourinho na pia kushinda mchezo wa kwanza Uwanja wa Old Trafford tangu mwaka 2006.
  Arsene Wenger hana uhakika wa kumuanzisha mshambuliaji wake, Alexis Sanchez baada ya kuumia nyama za paka akiichezea nchi yake, Chile wiki hii katika mechi ya kufuzu Kombe la Dunia, hivyo yuko chini ya uangalizi wa dawati la tiba la Arsenal. 

  Arsene Wenger na Jose Mourinho wanakutana tena leo katika Ligi Kuu ya England  PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Majeruhi wengine Arsenal ni Santi Cazorla, Lucas Perez, Per Mertesacker na Danny Welbeck ambao wotev watakosekana leo.
  Man United nayo itamkosa Hector Bellerin ambaye kwa takriban mwezi sasa anasumbuliwa na maumivu ya kifundo cha mguu aliyoyapata katika mchezo na Tottenham
  Manchester United imepoteza mechi moja tu kati ya 10 zilizopita za Ligi Kuu dhidi ya Arsenal, ikifungwa 3-0 Uwanja wa Emirates Oktoba 2015.
  Arsenal imefikisha miaka 10 ya kucheza bila kushinda Uwanja wa Old Trafford, mara ya mwisho ikiwafunga Mashetani Wekundu Septemba mwaka 2006, bao la ushindi likifungwa na Emmanuel Adebayor.
  Manchester United imetoa sare mechi zote mbili zilizopita za Ligi Uwanja wa Old Trafford – mara ya mwisho kwoa kutoa sare tatu mfululizo nyumbani ilikuwa Aprili mwaka 1992.
  Arsenal imepoteza mechi 22 dhidi ya Manchester United kwenye Ligi Kuu – ambayo ni idadi kubwa ukilinganisha na dhidi ya timu nyingine, huku mechi 15 kati ya hizo ikifungwa Old Trafford.
  Jose Mourinho hajawahi kufungwa na Arsenal mechi ya Ligi Kuu, akishinda tano na kutoa sare sita kati ya 11 zilizopita dhidi ya The Gunners.
  Ushindi pekee wa Arsene Wenger katika mechi 15 zilizopita kama kocha dhidi ya timu yoyote ya Jose Mourinho ulikuwa ni mwaka 2015 kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii.
  Wenger amekuwa akipoteza kila mechi anayokutana na Manchester United ikiwa chini ya kocha mpya katika Ligi Kuu mbele ya Sir Alex Ferguson Novemba 1996, David Moyes Novemba 2013 na Louis Van Gaal  Novemba 2014.
  Wayne Rooney amefunga mabao 14 kwenye mechi za mashindano yote dhidi ya Arsenal katika kipindi chake cha kuwa Man United; idadi ambayo inazidiwa na mabao aliyofunga dhidi ya Aston Villa tu (15) ni ni sawa na mabao aliyofunga dhidi ya Newcastle United, 14 pia.
  Rooney alifunga bao lake la kwanza kabisa katika Ligi Kuu ya England Oktoba 2002 na bao lake ka kwanza dhidi ya Arsenal katika Ligi Kuu alifunga akiwa Man United lilikuja Oktoba 2004 na bao lake la 100 katika Ligi Kuu alifunga Januari 2010 dhidi ya The Gunners. Anahitaji mabao mawili zaidi kumfikia Sir Bobby Charlton aliyefunga mabao 249 na kuwa mfungaji bora wa muda wote wa Manchester United.
  Arsenal ni moja kati ya timu mbili za Ligi Kuu ambazo hazijaruhusu nyavu zake kutikiswa ndani ya dakika 15 za mwanzo msimu huu pamoja na West Bromwich Albion.
  Mechi nyingine za Ligi Kuu ya England leo ni kati ya Everton na Swansea City Uwanja wa Goodison Park Saa 12:00 jioni sawa na Watford na Leicester City Uwanja wa Vicarage Road, Crystal Palace na Manchester City Uwanja wa Selhurst Park, Stoke City na AFC Bournemouth Uwanja wa Britannia, Sunderland na Hull City Uwanja wa Light, Southampton na Liverpool Uwanja wa St. Mary's na Tottenham Hotspur dhidi ya West Ham United Saa 2:30 usiku Uwanja wa White Hart Lane.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WENGER NA MOURINHO KAZI IPO LEO MAN U NA ARSENAL OLD TRAFFORD Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top