• HABARI MPYA

  Sunday, November 13, 2016

  UGANDA YAILAZA KONGO 1-0 MECHI YA KUFUZU KOMBE LA DUNIA

  TIMU ya taifa ya Uganda, The Cranes jana imepanda kileleni mwa Kundi E kuwania tiketi ya Kombe la Dunia amwaka 2018 Urusi baada ya kuifunga Kongo Brazzaville 1-0 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Taifa wa Mandela, Namboole.
  Asante kwake, kiungo wa Standard Liege ya Ubelgiji, Faruku Miya aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 19.
  Uganda ilipata pigo katika mchezo huo dakika ya 10 tu baada ya beki wake tegemeo, Juuko Murshid kupasuka kichwani na nafasi yake kuchukuliwa na William Luwagga Kizito anayechezea Rio Ave ya Ureni na Hassan Wasswa Mawanda akaenda kucheza katikati.
  Kikosi cha Uganda kabla ya mchezo wa jana Uwanja wa Taifa wa Mandela, Namboole mjini Kampala

  Kipindi cha pili, Michael Azira akampisha Tonny Mawejje dakika ya 60, kabla ya Godfrey Walusimbi kuchukua nafasi ya Moses Oloya zikiwa zimebaki dakika 10.
  Kikosi cha Uganda kilikuwa; Robert Odongkara, Nicholas Wakiro  Wadada, Joseph Ochaya, Isaac Isinde, Juuko Murshid/William Luwagga Kizito dk10, Hassan Wasswa Mawanda , Khalid Aucho, Tonny Mawejje/Michael Azira dk60, Moses Oloya/Godfrey  ‘Jajja Walu’ Walusimbi dk85, Geoffrey Massa na Faruku Miya
  Kongo Brazzaville; Wolfij Mongondza, Itova Berangez, Marvin Baudry, Bous Moubhio, Carof Bakoua, Dore Ferebory/Mbossy Ganyoula dk45, Bouka  Moutou/Ismaael Ankombo dk87, Jordan Massengo, Tsiba Kessel/Stanslas Ankra dk46, Dzon Delarge na N Dockyt Mesou.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: UGANDA YAILAZA KONGO 1-0 MECHI YA KUFUZU KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top