• HABARI MPYA

  Saturday, November 12, 2016

  TUNISIA YAIBWAGA LIBYA ALGERIA 1-0

  BAO pekee la Wahbi Khazri juzi usiku lilitosha kuipa ushindi wa 1-0 Tunisia dhidi ya Libya waliokuwa pungufu ya mchezaji mmoja katika mchezo wa Kundi A kuwania tiketi ya Kombe la Dunia mwaka 2018 nchi Urusi, uliofanyika Uwanja wa Omar Hamadi mjini Algiers.
  Kutokana na vurugu za kisiasa nchini kwao, Libya sasa wanacheza mechi zao nje ya nchi yao. Ikitoka kushinda mechi ya kwanza dhidi ya Guinea 2-0, Tunisa ilizidi kupaa dhidi ya wapinzani wao Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambao watakuwa ugenini mjini Conakry leo.
  Wahbi Khazri alifunga bao pekee juzi Tunisia ikiilaza 1-0 Libya Uwanja wa Omar Hamadi mjini Algiers

  Ali Salama siyo tu alisababisha penalti, lakini pia alitolewa kwa kadi nyekundu na kuiponza Libya kubaki na wachezaji 10 uwanjani.
  Kiungo wa Sunderland, Khazri, alikwenda kufunga kwa penalti ambayo ilikaribia kuokolewa na kipa Muhammad Nashnoush aliyeugusa kwa vidole mpira.
  Kikosi cha Libya kilikuwa: Nashnoush; Salama, Mounir/Khamaj dk 74, Fetori, Gamal, Benali/Tabal dk 59, Sabbou, El Masrati, Al Masri, Al-Warfali na Saltou/Zubya dk 62.
  Tunisia: Mathlouthi; Abdennour, Maaloul, Dhaouadi, Mohsni, Nagguez, Khazri/Bguir dk83, Sassi, Ben Amosr, Ben-Hatira/Sliti dk 46 na Khenissi/Harbaoui dk 90+2.  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TUNISIA YAIBWAGA LIBYA ALGERIA 1-0 Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top