• HABARI MPYA

  Tuesday, November 08, 2016

  TASWA WAMLILIA MWENYEKITI AZAM

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  CHAMA Cha waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), kimepokea kwa masikitikio makubwa taarifa za kifo cha Mwenyekiti wa klabu ya Azam FC na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu, Sheikh Said Muhammad Abeid, kilichotokea  jana alasiri katika Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam.
  Sheikh Said Muhammad Abeid anazikwa jioni ya leo makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam 

  Katibu wa TASWA, Amir Mhando amesema leo katika taarifa yake kwamba Mzee Said atakumbukwa na waandishi wa habari za michezo kutokana na ukaribu wake na wanahabari na alikuwa na ushirikiano wa kutosha pale alipoombwa kufanya hivyo,  alikuwa kiungo kikubwa kwa TASWA kufanikisha matukio mbalimbali ya udhamini.
  Mhando amesema TASWA inatoa pole kwa familia ya marehemu, klabu ya Azam na wanamichezo wote hapa nchini katika kuomboleza kifo cha Mzee Said, huku tukiwatakia moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.
  "Itoshe kusema tumepoteza mtu muhimu sana, ambaye  mchango wake na uhodari havitasahaulika kwa wadau wa michezo," alisema Amir Mhando.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TASWA WAMLILIA MWENYEKITI AZAM Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top