• HABARI MPYA

  Sunday, November 13, 2016

  TAIFA STARS YACHEZEA 3-0, SAMATTA 'AFICHWA' HARARE

  Na Mwandishi Wetu, HARARE
  TIMU ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars jioni ya leo imefungwa mabao 3-0 na Zimbabwe katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa jana Uwanja wa Taifa, Harare, Zimbabwe.
  Kwa ujumla Taifa Stars, inayofundishwa na Nahodha wake wa zamani, Charles Boniface Mkwasa imecheza ovyo leo na ilistahili kipigo hicho.
  Mshambuliaji wa K.V. Oostende ya Ubelgiji, Knowledge Musona aliifungia Zimbabwe bao la kwanza dakika ya tisa, kabla ya mshambuliaji wa Helsingborgs IF ya Sweden, Matthew Rusike kufunga bao la pili dakika ya 53 na mshambuliaji wa Dalian Yifang ya China, Nyasha Mushekwi kufunga la tatu dakika ya 56.
  Mbwana Samatta anayechezea KRC Genk ya Ubelgiji alidhibitiwa vikali na mabeki wa Zimbabwe

  Nahodha wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta KRC Genk ya Ubelgiji alidhibitiwa vikali sawa na mchezanji mwenzake wa zamani wa TP Mazembe ya DRC, Thomas Ulimwengu. 
  Kikosi cha Taifa Stars  jana kilikuwa; Aishi Manula, Michael Aidan, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Erasto Nyoni, Andrew Vincent, Himid Mao, Simon Msuva/Thomas Ulimwengu dk69, Muzamil Yassin/Mohammed Ibrahim dk69, Mbwana Samatta, Elius Maguri/John Bocco dk72 na Shizza Kichuya.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TAIFA STARS YACHEZEA 3-0, SAMATTA 'AFICHWA' HARARE Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top