• HABARI MPYA

  Saturday, November 12, 2016

  TAIFA STARS NA ZIMBABWE LIVE KESHO AZAM TV

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MCHEZO wa kirafiki wa kimataifa kati ya wenyeji, Zimbabwe na Tanzania kesho utaonyeshwa moja kwa moja na Televisheni ya taifa ya nchi hiyo, ZBC.
  Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas aliyeongozana na Taifa Stars nchini Zimbabwe, amesema kwamba timu ZBC nao wameipa haki Azam TV ya Tanzania kuonyesha pia mchezo pia.
  "Kituo cha Televisheni ya Taifa hapa Zimbabwe (ZBC) na huko nyumbani wataungana na Kituo cha Televisheni cha Azam ( Azam Tv) inayopatikana kwenye king'amuzi cha Azam muda wote wa mchezo kuonyesha mchezo huo," alisema Alfred Lucas.
  Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta ataiongoza timu kesho Uwanja wa Taifa wa Harare kumenyana na wenyeji, Zimbabwe katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa 

  Taifa Stars itashuka kwenye Uwanja wa Taifa wa Harare kesho jioni kumenyana na wenyeji, Zimbabwe katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa. 
  Stars imefikia kwenye hoteli ya The Rainbow Towers mjini Harare na mchezo wa kesho utaanza Saa 9.00 Alasiri kwa saa za Zimbabwe, sawa na saa 10.00 jioni kwa saa za Tanzania. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TAIFA STARS NA ZIMBABWE LIVE KESHO AZAM TV Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top