• HABARI MPYA

  Tuesday, November 08, 2016

  STRAIKA LA MEDEAMA LAJA KUONGEZA NGUVU AZAM FC

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI wa Medeama SC ya Ghana, Bernard Ofor yuko mbioni kujiunga na Azam FC ya Dar es Salaam baada ya makubaliano ya awali.
  Mchezaji huyo wa zamani wa New Edubiase United ameondoka Ghana jana na anatarajiwa kuwasili Dar es Salaam leo kumalizana washindi hao wa Ngao ya Jamii.
  Bernard Ofor anakuja Dar es Salaam kujiunga na klabu ya Azam FC kutoka Medeama SC ya Ghana

  Akifanikiwa kusaini Azam FC, Ofori ataungana na wachezaji wengine wawili wa Medeama SC waliojiunga na Azan FC, ambao ni winga Enoch Atta Agyei na mshambuliaji Daniel Amoah.
  Amoah amekwishajiunga na kikosi cha Azam FC kilicho chini ya kocha Mkuu, Mspaniola Zeben Hernandez Rodriguez wakati Agyei atajiunga na timu hiyo Januari atakapofikisha umri wa miaka 18.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: STRAIKA LA MEDEAMA LAJA KUONGEZA NGUVU AZAM FC Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top