• HABARI MPYA

  Sunday, November 06, 2016

  SIMBA WAPO UHURU LEO, YANGA SOKOINE TENA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea leo kwa vigogo Simba na Yanga SC kujitupa viwanjani kusaka pointi.
  Mabingwa watetezi, Yanga watakuwa wanajiuliza mbele ya Prisons Uwanja wa Sokoine, Mbeya wakati vinara wa ligi hiyo, Simba SC watajaribu kuendeleza wimbi la ushindi mbele ya African Lyon Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
  Jumatano Yanga walifungwa 2-1 na Mbeya City Uwanja wa Sokoine, Mbeya wakati Simba SC waliilaza Stand Unitedb 1-0 Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.
  Simba SC watakuwa wa shughuli na African Lyon leo Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam

  Na baada ya matokeo hayo, Ligi Kuu inaendelea leo kwa timu 12 kuchuana kwenye viwanja sita- ikiwemo hizo mechi mbili za vigogo wa soka nchini, Simba na Yanga.
  Mechi nyingine, Mbao FC watakuwa wenyeji wa Azam FC Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza, Ndanda watakuwa wenyeji wa Stand United ya Shinyanga Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara na Kagera Sugar wataikaribisha Ruvu Shooting Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
  Mechi nyingine, JKT Ruvu watakuwa wenyeji wa Toto Africans Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani wakati Jumatatu Mtibwa Sugar wataialika Mbeya City kwenye Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro na Mwadui watakuwa wenyeji wa Majimaji ya Songea Uwanja wa Mwadui, Shinyanga.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA WAPO UHURU LEO, YANGA SOKOINE TENA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top