• HABARI MPYA

    Wednesday, November 09, 2016

    SIMBA SC NA PRISONS SHUGHULI PEVU SOKOINE LEO

    Na Mwandishi Wetu, MBEYA
    VINARA wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simba SC leo wanakamilisha mechi zao za mzunguko wa kwanza kwa kumenyana na wenyeji, Prisons Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
    Timu hiyo ya kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog ipo Mbeya tangu Jumatatu mara tu baada ya mchezo wao uliopita wakifungwa 1-0 na African Lyon Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
    Na wachezaji wa Simba wamepania kushinda mechi hiyo ili kumaliza vizuri mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu.
    Mechi nyingine ya leo ni kati ya Mwadui ya Shinyanga na Azam FC ya Dar es Salaam ambayo itachezwa Uwanja wa Mwadui, Shinyanga, wakati kesho ligi hiyo itaendelea kwa mchezo mmoja tu, Yanga SC wakimenyana na Ruvu Shooting Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
    Awali pamoja na mechi hizo kuwekwa kwenye ratiba, lakini hazikuwa na tarehe huku ikielekezwa tarehe zitatajwa baadaye. 
    Tayari Bodi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), imewasiliana na wahusika kuhusu mabadiliko hayo. Sababu ya kuvuta nyuma michezo hiyo ni kutoa nafasi ya maandalizi ya kambi ya timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayotarajiwa kusafiri Ijumaa wiki hii kwenda Harare Zimbabwe kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa unaotarajiwa kufanyika Novemba 13, maka huu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC NA PRISONS SHUGHULI PEVU SOKOINE LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top