• HABARI MPYA

  Monday, November 14, 2016

  SERENGETI BOYS YAPATA SARE UGENINI NA TIMU YA KOREA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 – Serengeti Boys, imeanza jana imelazimisha sare ya bila kufungaa na wenyeji ⁠Seongnam FC katika ziara yake ya Korea Kusini.
  Serengeti ambayo iko huko kwa mwaliko wa Shirikisho la Soka la Korea Kusini, itarejea wiki ijayo na kukutana na mchezo mwingine wa dhidi ya nyota 40 walioteuliwa na Airtel baada ya michuano ya Kampuni hiyo ya simu iliyofanyika mwaka huu kwenye kona mbalimbali nchini kabla ya fainali zake kufanyika Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
  Serengeti Boys baada ya mechi yao na ⁠Seongnam FC katika ziara yake ya Korea Kusini

  Serengeti Boys imepata nafasi hiyo kutokana na umahiri wake wa kucheza soka la ushindani kwani kwa kipindi cha mwaka mmoja tu, imeweza kucheza michezo 16 ya kimataifa ambako imekuwa ikifanya vema katika mechi 15 kabla ya 16 iliyopoteza dhidi ya Congo-Brazaville katika michuano ya kuwania nafasi ya kucheza Kombe la Mataifa ya Afrika.
  Kikosi cha Serengeti Boys kilichopo huko kinaundwa na makipa Ramadhani Kabwili, Kelvin Kayego na Samwel Brazio; mabeki ni Shomari Ally, Israel Mwenda, Nickson Kibabage, Dickson Job, Ally Msengi na Enrick Vitalis wakati viungo ni Ally Ng’anzi, Shaban Ada, Asad Juma, Issa Makamba huku washambuliaji wakiwa ni Muhsin Makame, Ramadhani Gadaffi, Rashid Chombo, Cyprin Mtesigwa na Mohammed Abdallah.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SERENGETI BOYS YAPATA SARE UGENINI NA TIMU YA KOREA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top