• HABARI MPYA

  Saturday, November 05, 2016

  PHIRI: NITAWAFUNGA NA MTIBWA KESHO KUTHIBITISHA SIKUWABAHATISHA YANGA

  Na David Nyembe, MBEYA
  KOCHA Mmalawi wa Mbeya City, Kinnah Phiri amesema kwamba ataifunga Mtibwa kesho ili kuthibitisha hakubahatisha kuifunga Yanga Jumatano.
  Baada ya ushindi wa 2-1 Jumatano nyumbani, Mbeya City watashuka tena kesho Uwanja wa Manungu, Turiani mjini Morogoro kumenyana na wenyeji, Mtibwa Sugar kukamilisha mechi zao za mzunguko wa kwanza.
  Na akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE jana, kocha Phiri alisema kwamba ushindi huo aliutarajia baada ya maandalizi mazuri, hivyo hakubahatisha.
  “Wachezaji wengi wa Mbeya City ni wapya hivyo walikuwa wanajaribu kushika mafundisho yangu taratibu na nina furaha wanajifunza kwa kasi na hadi kufika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu watakuwa wameiva kabisa. Nina furaha walicheza kwa kufuata maelekezo yangu,”alisema Phiri.
  Kocha Kinnah Phiri amesema kwamba ataifunga Mtibwa kesho ili kuthibitisha hakubahatisha kuifunga Yanga Jumatano

  Mabao ya MCC Jumatano yalifungwa na Hassan Mwasapili dakika ya sita na Nahodha Kenny Ally dakika ya 36, wakati la Yanga lilifungwa na Mzimbabwe, Donald Ngoma dakika ya 45 na ushei.
  Ushindi huo wa kwaza kwa Mbeya dhidi ya Yanga tangu wapande Ligi Kuu, unaifanya MCC ifikishe pointi 19 baada ya kucheza mechi 14, wakati Yanga inabaki na pointi zake 27 za mechi 13.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PHIRI: NITAWAFUNGA NA MTIBWA KESHO KUTHIBITISHA SIKUWABAHATISHA YANGA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top