• HABARI MPYA

  Monday, November 14, 2016

  OMOG, KAHEMELE KUMVUTA KIPRE BALOU SIMBA SC?

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIUNGO Muivory Coast, Kipre Michael Balou anaweza akajiunga na Simba baada ya kutemwa na Azam FC aliyotumikia tangu mwaka 2011.
  Inaaminika Balou ni kipenzi cha kocha wa sasa wa Simba, Mcameroon Joseph Marius Omog baada ya kufanya naye kazi awali Azam FC.
  Lakini pia, Katibu Mkuu wa Simba, Patrick Kahemele inaaminika ni shabiki mzuri wa Balou na ndiye aliyefanikisha usajili wake pamoja na nduguye, Kipre Tchetche mwaka 2011. Tchetche ameondoka Azam FC msimu huu kwenda Oman.
  Kipre Balou anaweza kuhamia Simba baada ya kutemwa na Azam FC aliyotumikia tangu mwaka 2011

  Azam FC imevunja mkataba na Balou baada ya mapendekezo ya benchi la ufundi chini ya Kocha Mkuu, Zeben Hernandez Rodriguez na kwa ujumla inataka kukata wachezaji wawili wa kigeni kutoa nafasi ya wachezaji wengine wa kigeni kusajiliwa.
  Wachezaji wengine wa kigeni Azam FC ni Francesco Zekumbawira, Bruce Kangwa kutoka Zimbabwe, Ya Thomas Renaldo, Serge Wawa Pascal kutoka Ivory Coast, Daniel Amoah wa Ghana na Jean Baptiste Mugiraneza kutoka Rwanda.
  Tayari Azam FC imemsajili winga Mghana, Enock Atta Agyei kutoka Medeama SC ya Ghana na wakati huo huo wachezaji wengine saba wamefika kwa majaribio kutokaa nchi tofauti.
  Hao ni Mbimbe Aaron Nkot, Kingue Mpondo Stephane, Yaya Awaba Joel kutoka Cameroon, Kone Nabil Ibrahim, Konan Oussou kutoka Ivory Coast, Samuel Afful na Benard Ofori wote kutoka Ghana.
  Hata hivyo, kwa Simba nayo ili kumsajili Balou italazimika kuacha mchezaji, kwani imekamilisha wachezaji saba wa kigeni kwa mujibu wa kanuni.
  Hao ni kipa Vincent Angban, Frederick Blagnon kutoka Ivory Coast, Janvier Bokungu, Mussa Ndusha kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Method Mwanjali kutoka Zimbabwe, Juuko Murshid kutoka Uganda na Laudit Mavugo kutoka Burundi. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: OMOG, KAHEMELE KUMVUTA KIPRE BALOU SIMBA SC? Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top