• HABARI MPYA

    Wednesday, November 02, 2016

    NGOMA LEO ANAANZA YANGA NA MBEYA CITY SOKOINE

    Na Mwandishi Wetu, MBEYA
    MZAMBIA Obrey Chirwa leo ameanzishiwa benchi Yanga ikimenyana na Mbeya City Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
    Kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm amewaanzisha pamoja leo washambuliaji Mrundi Amissi Tambwe na Mzimbabwe, Donald Ngoma katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
    Kwa ujumla Pluijm amerudi na kikosi kile kile kilichoifunga Mbao FC 3-0 Jumapili Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam tofauti ni Ngoma tu kuanza badala ya Chirwa. 
    Leo Donald Ngoma anaanza Yanga na Mbeya City Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya

    Kikosi cha Yanga leo ni; Deogratius Munishi 'Dida', Hassan Kessy, Mwinyi Hajji, Andrew Vincent, Vincent Bossou, Mbuyu Twite, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Amissi Tambwe, Donald Ngoma na Deus Kaseke
    Katika benchi wapi; Beno Kakolanya, Kevin Yondan, Oscar Joshua, Thabani Kamusoko, Juma Mahadhi, Obrey Chirwa na Geoffrey Mwashiuya.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NGOMA LEO ANAANZA YANGA NA MBEYA CITY SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top