• HABARI MPYA

  Thursday, November 03, 2016

  NGASSA AREJEA NYUMBANI KWA MATATIZO YA KIFAMILIA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania, Mrisho Khalfan Ngassa anatarajiwa kurejea nyumbani kwa matatizo ya kifamilia.
  Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE leo kwa simu kutoka Muscat, Oman, Ngassa alisema kwamba amepata matatizo ya kifamilia na atakuja nchini kwa muda baada ya kuruhusiwan na klabu yake Fanja.
  “Nimeruhusiwa, nitakuwa huko siku mbili hizo,”alisema Ngassa ambaye amejiunga na Fanja Septemba mwaka huu na kuongeza; “Kuna mambo mengine yanatokea katika familia hakuna namna nyingine zaidi ya kuacha kazi na kwenda kushiriki,”.
  Mrisho Ngassa (kulia) anatarajiwa kurejea nyumbani kwa matatizo ya kifamilia

  Aidha, Ngassa alisema wakati anajiandaa kwa safari ya kurudi nyumbani kwa matatizo ya kifamilia, aliumia mazoezini hivyo atakapaokuwa Tanzania itabidi atibiwe kabisa ili arejee Oman akiwa fiti.
  “Ningesema nitibiwe kwanza kule ndiyo nirudi nyumbani, ningechelewa, kwa hiyo nimewaomba wakati nikiwa huku nitibiwe kabisa ndiyo nirudi. Kwa hiyo ninaweza kukaa kidogo kama wiki hivi,”alisema.
  Tayari Ngassa amefunga bao moja katika mchezo wa Ligi Kuu ya Oman, Fanja ikilazimishwa sare ya 1-1 na Al-Nahda Uwanja wa Seeb, Muscat.
  Ngassa alijiunga na Fanja mwezi uliopita kwa mkataba wa miaka miwili akitokea ya Free State Stars ya Afrika Kusini, baada ya kuomba mwenyewe kuvunja Mkataba.
  Ngassa alijiunga na Free State Stars Mei mwaka jana akisajiliwa na kocha Mmalawi, Kinnah Phiri kwa mkataba wa miaka minne.
  Hata hivyo, kocha aliyemsajili baba huyo wa Farida (9) na Faria (7) alifukuzwa baada ya miezi miwili tu na sasa tayari yuko Mbeya City ya Tanzania.
  Katika kipindi cha mwaka mmoja wa kuwa Free State, Ngassa alifanya kazi na makocha wanne akiwemo huyu wa sasa, Mfaransa Denis Lavagne aliyeanza kazi Juni mwaka huu.
  Wengine ni Mjerumani Ernst Middendorp aliyefanya kazi kati ya Septemba na Desemba 2015, Mtaliano Giovanni Solinas aliyefanya kazi kati ya Desemba na Mei 2016.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NGASSA AREJEA NYUMBANI KWA MATATIZO YA KIFAMILIA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top