• HABARI MPYA

  Tuesday, November 08, 2016

  MZEE BAKHRESA AONGOZA MAZISHI YA MWENYEKITI AZAM

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MAMIA ya wadau wa soka jioni ya leo wameshiriki mazishi za aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Sheikh Said Muhammad Abeid aliyefariki juzi jioni Dar es Salaam.
  Sheikh Said aliyekuwa pia Mwenyekiti wa klabu ya Azam FC, alizikwa katika makaburi ya Kisutu, jirani na msikiti wa Maamour, Upanga ambako mwili wake ulisaliwa baada ya sala ya Alasiri.
  Mwenyekiti wa makampuni ya Bakhresa Group, wamili wa Azam FC, Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa alihudhuria mazishi hayo pamoja na wanawe wakiwemo, Mkurugenzi Mkuu wa makampuni hayo, Abubakar.
  Mzee Bakhresa (kushoto) alikuwepo kwenye mazishi ya Mzee Said leo makaburi ya Kisutu


  Jeneza lililobeba mwili wa marehemu Said likiteremshwa kaburini leo
  Jeneza likipelekwa ndani ya makaburi ya Kisutu baada ya kuwasili kutoka msikiti wa Maamour 
  Umati wa waliojitokeza katika safari ya mwisho ya Sheikh Said Muhammad
  Yussuf Bakhresa (kulia) naye alikuwepo makaburi ya Kisutu leo

  Sura za viongozi wa klabu na vyama mbalimbali vya michezo nchini, wanachama maarufu wa klabu za soka na wafanyakazi wa makampuni mbalimbali ya Bakhresa Group wakiwemo wachezaji wa timun za vijana na Azam ndizo zilizotawala wakati wa mazishi hayo.
  Wachezaji wa kikosi cha kwanza chab Azam FC hawakuwepo kwa sababu wapo na timu hiyo Mwadui, Shinyanga kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na wenyeji, Mwadui kesho.  
  Sheikh Said Muhammad Abeid alifariki dunia jana jioni katika hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam, saa chache baada ya kufikishwa kwa matibabu.
  Sheikh Said alizaliwa Machi 20 mwaka 1940 visiwani Zanzibar na anatarajiwa na enzi za ujana wake alicheza soka na Kriketi.
  Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Sheikh Said Muhammad Abeid mahali pema peponi, Amin.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MZEE BAKHRESA AONGOZA MAZISHI YA MWENYEKITI AZAM Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top