• HABARI MPYA

  Friday, November 11, 2016

  MBUNGE REFA WA ZAMANI 'YANGA DAMU' AFARIKI DUNIA DODOMA

  Na Mwandishi Wetu, DODOMA
  REFARII maarufu wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Hafidh Ally Tahir (pichani kushoto) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya General mjini Dodoma alikopelekwa kwa matibabu. 
  Hafidh aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Dimani, Zanzibar (CCM), enzi zake miaka ya 1980 na 1990 alikuwa refa wa kiwango cha juu nchini kiasi cha kufikiwa kuvikwa beji ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
  Pamoja na hayo, Hafidh alikuwa mpenzi mzuri na mwanachama wa klabu ya Yanga na ni jana tu alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Tawi la Yanga Bungeni mjini Dodoma chini ya Uenyekiti wa Venance Mwamoto, na Makamu Ridhiwani Kikwete.
  Hafidh alizaliwa Oktoba 30, mwaka 1953 visiwani Zanzibar na aliwahi kuwa Mkuu wa Sauti ya Tanzania Zanzibar (1970-1978) na amekuwa mbunge tangu 2005 hadi mauti yanamkuta.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MBUNGE REFA WA ZAMANI 'YANGA DAMU' AFARIKI DUNIA DODOMA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top