• HABARI MPYA

  Sunday, November 06, 2016

  MAZEMBE MABINGWA KOMBE LA SHIRIKISHO

  MABAO mawili ya kiungo Rainford Kalaba na mengine ya Merveille Bope na Jonathan Bolingi yametosha kuipa TP Mazembe ushindi wa 4-1 dhidi ya MO Bejaia leo katika mchezo wa marudiano wa fainali ya Kombe la Shirikisho Uwanja wa Mazembe mjini Lubumbashi, DRC.
  Sofiane Khadir aliifungia timu ya Algeria bao la kufutia machozi na kufanya matokeo ya jumla yawe 5-2 baada ya sare ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita mjini Blida.
  ‘Les Corbeaux’ inafuata nyayo za Al Ahly ya Misri kutwaa Kombe la Ligi ya Mabingwa na Shirikisho mfululizo. Ahly ilifanya hiyvo mwaka 2013 na 2014 wakati Mazembe imefanya hivyo mwaka jana na mwaka huu.
  Mbali na kupewa taji, Mazembe walizawadiwa pia dola 660,000 huku wapinzani wao, Bejaia wakipewa dola 462,000.
  Mazembe sasa watamenyana na washindi wa Ligi ya Mabingwa, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini kati ya Februari 17 na 19 mwakani kuwania taji la Super Cup ya CAF.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAZEMBE MABINGWA KOMBE LA SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top