• HABARI MPYA

    Saturday, November 12, 2016

    KADITO AINGIA MKATABA WA UWAKALA NA TIMU YA RAIS WA FFB

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KLABU ya Aigle Noir inayomilikiwa na Rais wa Shirikisho la Soka Burundi (FFB), Reverien Ndikuriyo, imeingia makubaliano na Mtanzania, Dennis Kadito kuwa wakala wao kwa miaka 10.
    Akizungvumza na BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE leo kwa simu kutoka Uholanzi anakoishi, Kadito amesema kwamba katika mkataba wake na Aigle Noir kazi yake itakuwa ni kusimamia maslahi ya timu katika haki zake hususan uhamisho wa wachezaji. “Pia mimi ninakuwa wakala kwa ajili ya wachezaji walio chini ya Aigle Noir kwa watakaopenda niwasimamie,”alisema Kadito.
    Mtanzania, Dennis Kadito (kushoto) akisaini mkataba na mmiliki wa Aigle Noir, Reverien Ndikuriyo ambaye ni Rais wa FFB
    Kadito atakuwa wakala wa Aigle Noir kwa miaka 10 kwa mujibu wa mkataba waliosaini 

    Kadito alisema kwamba amevutiwa na mipango mizuri ya uendeshwaji wa timu hiyo, hivyo amekubali kushirikiana nayo.
    “Jamaa wana mipango mizuri, wanajenga Uwanja kwa ajili ya shule za msingi ma sekondari. Na zaidi ya mpira wa miguu, Aigle Noir itajikita katika kukuza vipaji vya mpira wa kikapu, riadha na michezo mingine,”alisema.
    K⁠⁠⁠adito alisema pamoja na hayo, kazi nyingine ni kutoa vipaji kutoka Burundi kwenda nchi nyingine, kusimamia mikataba ya wachezaji walio chini yake na pia kusimamia maslahi ya Aigle Noir.
    “Nitashughulikia pia ushirikiano wa kimataifa kwa mambo ya mpira katika kuendelezea klabu ya Aigle Noir na faida kwa wachezaji wa Burundi kwa ujumla,”alisema Kadito.
    Kadito ni Mtanzania anayesifika kwa kuwasaidia wachezaji wengi wa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kupata timu za kuchezea Ulaya na nchi nyingine za Afrika zilizopiga hatua kwenye soka ya kulipwa kama za Kaskazini mwa Afrika na Afrika Kusini.
    Kwa nyumbani Tanzania, Kadito anakumbukwa zaidi kwa kumpatia timu Ufaransa beki Shomary Kapombe. Mwaka 2014 Kapombe alisajiliwa AS Cannes ya Daraja la Sita Ufaransa, lakini baada ya miezi kadhaa mchezaji huyo wakati huo akitokea Simba SC akaamua kurudi nyumbani na kusaini Azam anakoendelea kucheza hadi sasa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KADITO AINGIA MKATABA WA UWAKALA NA TIMU YA RAIS WA FFB Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top