• HABARI MPYA

  Thursday, November 03, 2016

  JAMAA LAWAPIGA TANO PEKE YAKE AKINA SAMATTA WALALA 5-3 UGENINI ULAYA

  Na Mwandishi Wetu, GENK
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta amecheza kwa dakika 83 timu yake, KRC Genk ikifungwa 5-3 na Athletic Bilbao Uwanja wa San Mames Barria mjini Bilbao katika mchezo wa Kundi F Europa League.
  Kwa matokeo hayo, Athletic Bilbao sasa inafikisha pointi sita sawa na KRC Genk kuelekea mechi za mwisho za makundi Novemba 24, mwaka huu wakati Sassuolo Rapid Wien zinafunga pia kwa pointi tano tano kila baada ya sare ya 2-2 leo. 
  Mabao ya Bilbao yote yalifungwa na mshambuliaji Mspaniola Aritz Aduriz Zubeldia dakika ya nane, 24, 44 na 94 kwa penalti na 74, wakati ya Genk yalifungwa na Leon Bailey dakika ya 28, Onyinye Wilfred Ndidi dakika ya 51 na Tino-Sven Susic dakika ya 79. 
  Genk itamaliza na Rapid Wien nyumbani Uwanja wa Cristal Arena Novemba 24, wakati Bilbao itamaliza na Sassuolo San Mames Barria siku hiyo hiyo.

  Mbwana Samatta (kushoto alimpisha mshambuliaji Mgiriki Nikolaos Karelis dakika ya 83 leo Genk ikilala 5-3

  Katika mchezo wa leo, Samatta alimpisha mshambuliaji Mgiriki Nikolaos Karelis dakika ya 83 baada ya kufanya shughuli pevu kwenye mchezo huo wa ugenini.
  Huo unakuwa mchezo wa 32 kwa Samatta tangu amejiunga na Genk Januari mwaka huu kutoka TP Mazembe ya DRC, 18 msimu uliopita na 13 msimu huu, akifunga mabao nane, matatu msimu huu na matano msimu uliopita.
  Katika mechi hizo, ni 17 tu ndiyo alianza, 10 msimu uliopita na tano msimu huu, wakati 14 alitokea benchi nane msimu uliopita na 11 msimu huu – na mechi 10 hakumaliza akitolewa, sita msimu uliopita na nne msimu huu.

  Aritz Aduriz Zubeldia amefunga mabao yote ya Athletic Bilbao wakishinda 5-3 dhidi ya Genk leo
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JAMAA LAWAPIGA TANO PEKE YAKE AKINA SAMATTA WALALA 5-3 UGENINI ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top