• HABARI MPYA

  Friday, November 18, 2016

  BIN ZUBEIRY ATEULIWA KAMATI YA FEDHA NA MIPANGO NDFA

  Na Mwandishi Wetu, MWANZA
  MTENDAJI Mkuu wa Bin Zubeiry Sports – Online, Mahmoud Zubeiry ameteuliwa kwenye Kamati ya Fedha Uchumi na Mipango ya Chama cha Soka Nyamagana, (NDFA) Mwanza.
  Uteuzi huo umefanywa na uongozi mpya wa NDFA chini ya Mwenyekiti wake, Munga Lupindo ambao una wiki moja tu tangu uingie madarakani. 
  Mbali na ‘bosi’ huyo wa tovuti namba moja ya michezo Tanzania, Zubeiry – wengine walioteuliwa kwenye Kamati hiyo ni Paresh Kotecha, Octavian Komba, Godfrey Kiango, Yassir Fuad Said, Bob Butambala na Kabole Kahungwa, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa NDFA.  
  Mahmoud Zubeiry ameteuliwa kwenye Kamati ya Fedha Uchumi na Mipango ya Chama cha Soka Nyamagana, (NDFA) Mwanza.

  Kamati nyingine iliyoundwa ni ya Ufundi, Vijana na Soka la Wanawake inayoundwa na Kessy Mziray, Kanuti Masanja, Juma Amiri Maftah, Job Mshumba, Tito Mkami, Mathias Wandiba na Wanniah Maulid.
  ⁠⁠K⁠⁠amati ya Waamuzi inaundwa na Frednand Chacha, Sebastian Lahani, Domicianus Valence, Isaac Wakuganda, Kamati ya Nidhamu na Rufaa inaundwa na Gasper Mwanalyela, Denis Kahangwa, Ernest Kijika na Khalid Bitebo ‘Zembwela’.
  Kamati mpya Utendaji ya NDFA ilipatikana baada ya uchaguzi wa Jumamosi iliyopita mjini Mwanza, Mwenyekiti akiingia Lupindo, Makamu Kahungwa, Katibu Mkuu Daddy Gilbert, Katibu Msaidizi Dominisius Valence, Mhasibu Shaaban Athumani, Mjumbe wa Mkutano Mkuu Isaac Wakuganda, Mjumbe wa Klabu Bob Butambala na Wajumbe Selemani Kiggi na Saidi Kizota.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BIN ZUBEIRY ATEULIWA KAMATI YA FEDHA NA MIPANGO NDFA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top