• HABARI MPYA

    Wednesday, November 02, 2016

    ANGBAN AWANIA BONGE LA REKODI SIMBA NA STAND UNITED LEO SHY

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    KIPA namba moja wa Simba SC, Vincent Atchouailou de Paul Angban leo atajaribu kucheza mechi ya sita bila kuruhusu nyavu zake kuguswa.
    Simba SC watakuwa wageni wa Stand United Uwanja wa Kambarage, Shinyanga leo katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. 
    Mara ya mwisho Angban alifungwa katika sare ya 1-1 na Yanga Oktoba 1, mwaka huu kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam bao la Amissi Tambwe.
    Tena bao lenyewe lilikuwa la utata, kwani Mrundi huyo kabla ya kumfunga kipa raia wa Ivory Coast aliuseti mpira kwa mkono, hilo bao la kuongoza kwa Yanga kabla ya Shizza Kichuya kuisawazishia Simba.

    'Simba One' Vincent Angban (katikati mbele) katika katika kikosi cha Wekundu wa Msimbazi

    Kutoka hapo, Angban akadaka mechi tano mfululizo bila kuruhusu bao, Simba ikishinda 2-0 dhidi ya Mbeya City Uwanja wa Sokoine, 2-0 na Kagera Sugar, 1-0 na Mbao, 3-0 na Toto Africans zote Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na 3-0 na Mwadui Uwanja wa Kambarage. 
    Kipa huyo wa zamani wa Chelsea FC ya England, alisajiliwa Simba SC msimu uliopita baada ya kufeli majaribio Azam FC, alikotua awali kujaribu bahati yake, lakini hakumvutia kocha Muingereza Stewart Hall aliyekuwa anaiongoza timu hiyo wakati huo.
    Lakini mbele ya Muigereza mwingine, Dylan Kerr aliyekuwa anaifundisha Simba SC msimu uliopita, Angaban akafuzu majaribio na kusajiliwa.
    Mlinda mlango huyo aliyezaliwa Februari 2, mwaka 1985 mjini Anyama, alikuja Tanzania akitokea klabu ya Ligi Kuu ya kwao, Ivory Coast, Jeunesse.
    Vincent Angban aliwahi kuchezea timu ya vijana ya Chelsea chini ya umri wa mika 21 ingawa alikuwa amevuka umri huo katika harakati za kutafuta kusajiliwa The Blues, lakini pamoja na kuonyesha uwezo Stamford Bridge, haikuwa bahati yake jezi ya bluu.
    Kipa huyo aliibukia katika klabu ya vijana ya Rio Sport d'Anyama kabla ya kupandishwa kikosi cha kwanza mwaka 2005, ambako hata hivyo miaka miwili baadaye aliondoka na kwenda kujiunga na Sawe Sports msimu wa 2006/2007.
    Mwaka 2007, Angban akajiunga na ASEC Mimosas ambako alikuwa kipa wa kwanza hadi mwanzoni mwa msimu wa 2009 alipoumia na nafasi yake kuchukuliwa na Daniel Yeboah. 
    Yeboah akawavutia zaidi makocha wa timu hiyo kwa ubora wake wa kuokoa michomo na akaendelea kudaka hata Angban alipopona.
    Baada ya kumaliza Mkataba wake ASEC, Angban akarejea Jeunesse na baadaye akaenda London kudakia U21 ya Chelsea.
    Amewahi kudakia timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Ivory Coast katika michuano ya Afrika nchini Benin mwaka 2005 na aliiwakilisha pia nchi yake katika Michezo ya Olimpiki mwaka 2008.
    Amedakia pia timu ya taifa ya wakubwa ya Ivory Coast ‘Tembo’ katika michuano ya CHAN ikiwemo ile ya mwaka 2009 na ndiye aliyesimama langoni katika mechi na Tanzania, Taifa Stars ikishinda 1-0 bao pekee la Mrisho Ngassa.   
    Kwa sasa Angban ndiye kipa namba moja Simba SC mbele ya chipukizi, Peter Manyika na Dennis Richard waliopandishwa kutoka timu ya vijana msimu uliopita.
    Na tangu ametua Simba SC, Angban amedaka jumla ya mechi 53 na kufungwa mabao 22 huku mechi 33 akisimama langoni bila kuruhusu nyavu zake kuguswa.

    Vincent Angban leo atajaribu kucheza mechi ya sita bila kuruhusu nyavu zake kuguswa

    REKODI YA VINCENT ANGBAN SIMBA SC
    Mechi Alizodaka;                       53
    Mabao aliyofungwa;                   22 
    Mechi alizodaka bila kufungwa; 33
    MECHI ZA VINCENT ANGBAN SIMBA SC
    Simba SC 4-0 Black Sailor (Aliingia kipindi cha pili hakufungwa, Kirafiki Zanzibar)
    Simba SC 2-0 Polisi (Hakufungwa, Kirafiki Zanzibar)
    Simba SC 3-0 Jang’ombe Boys (Hakufungwa, Kirafiki Zanzibar)
    Simba SC 3-2 KMKM (Aliingia kipindi cha pili, hakufungwa Kirafiki Zanzibar)
    Simba SC 1-0 SC Villa (Hakufungwa, Kirafiki Simba Day Taifa)
    Simba SC 0-0 Mwadui FC (Hakufungwa, alimpisha Dennis Richard dakika ya 35)
    Simba SC 0-2 JKU (Alifungwa mbili, Kirafiki Zanzibar)
    Simba SC 0-0 KVZ (Hakufungwa, Kirafiki Zanzibar)
    Simba SC 1-0 Mbeya City (Hakufungwa, Ligi Kuu Mbeya)
    Simba SC 0-1 Prisons (Alifungwa moja, Ligi Kuu Mbeya)
    Simba SC 1-0 Coastal Union (Hakufungwa, Ligi Kuu Mbeya)
    Simba SC 6-1 Majimaji FC (Alifungwa moja, Ligi Kuu Taifa)
    Simba SC 2-2 Azam FC (Alifungwa mbili, Ligi Kuu Taifa)
    Simba SC 1-1 Toto Africans (Alifungwa moja Ligi Kuu Kirumba)
    Simba SC 1-1 Mwadui FC (Alifungwa moja Ligi Kuu Kambarage)
    Simba SC 1-0 Ndanda FC (Hakufungwa, Ligi Kuu Nangwanda)
    Simba SC 1-0 Mtibwa Sugar (Hakufungwa, Ligi Kuu Taifa)
    Simba SC 2-0 JKT Ruvu (Hakufungwa, Ligi Kuu Taifa)
    Simba SC 3-0 Burkina Faso (Hakufungwa, Kombe la TFF Moro)
    Simba SC 4-0 African Sports (Hakufungwa, Ligi Kuu Taifa)
    Simba SC 5-1 Mgambo JKT (Alifungwa moja, Ligi Kuu Taifa)
    Simba SC 1-0 Kagera Sugar (Hakufungwa, Ligi Kuu Shinyanga)
    Simba SC 3-0 Kombaini ya Meatu (Hakufungwa, aliingia Kirafiki, Bariadi, Shinyanga)
    Simba SC 2-1 Stand United (Alifungwa moja, Ligi Kuu Shinyanga)
    Simba SC 0-2 Yanga SC (Alifungwa mawili, Ligi Kuu Taifa)
    Simba SC 5-1 Singida United (Alifungwa moja Kombe la TFF Taifa)
    Simba SC 2-0 Mbeya City (Hakufungwa Ligi Kuu Taifa) 
    Simba SC 3-0 Ndanda FC (Hakufungwa Ligi Kuu Taifa) 
    Simba SC 1-0 Prisons (Hakufungwa, Ligi Kuu Taifa) 
    Simba SC 2-0 Coastal Union (Hakufungwa, Ligi Kuu Mkwakwani, Tanga) 
    Simba SC 1-2 Coastal Union (Alifungwa mbili Kombe la TFF, Taifa) 
    Simba SC 0-1 Toto Africans (Alifungwa moja Ligi Kuu, Taifa) 
    Simba SC 3-0 Mafunzo (Hakufungwa, Kirafiki, Zanzibar) 
    Simba SC 0-0 Azam FC (Hakufungwa Ligi Kuu, Taifa) 
    Simba SC 0-1 Mwadui FC (Alifungwa moja, Ligi Kuu, Taifa) 
    Simba SC 6-0 Polisi Morogoro (Hakufungwa Kirafiki Morogoro).
    Simba SC 2-0 Moro Kids (Kirafiki Morogoro).
    Simba SC 0-1 KMC (alifungwa moja Kirafiki Morogoro).
    Simba SC 4-0 AFC Leopards (Hakufungwa Kirafiki Simba Day)
    Simba SC 1-1 URA (alifungwa moja Kirafiki Taifa)
    Simba 3-1 Ndanda (alifungwa moja Ligi Kuu Taifa)
    Simba 0-0 JKT Ruvu (Hakufungwa Ligi Kuu Taifa)
    Simba 2-0 Polisi Dodoma (Kirafiki Dodoma)
    Simba 2-1 Ruvu Shooting (alifungwa moja Ligi Kuu Uhuru)
    Simba 2-0 Mtibwa Sugar (Hakufungwa Ligi Kuu Uhuru)
    Simba  1-0 Azam (Hakufungwa Ligi Kuu Taifa)
    Simba 4-0 Maji Maji (Hakufunga Ligi Kuu Taifa)
    Yanga 1-1 Simba (Alifungwa moja Ligi Kuu Taifa)
    Simba 2-0 Mbeya City (Hakufungwa Ligi Kuu Sokoine) 
    Simba 2-0 Kagera Sugar (Hakufungwa  Ligi Kuu Uhuru)
    Simba 1-0 Mbao (Hakufungwa Ligi Kuu Uhuru)
    Simba 3-0 Toto Africans (Hakufungwa Ligi Kuu Uhuru)
    Simba 3-0 Mwadui (Hakufungwa Ligi Kuu Kambarage) 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ANGBAN AWANIA BONGE LA REKODI SIMBA NA STAND UNITED LEO SHY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top