• HABARI MPYA

  Wednesday, November 02, 2016

  ALGERIA YAITA KIPA MMOJA KUIVAA NIGERIA

  BEKI wa kati, Hicham Belkaroui  amerejeshwa kwenye kikosi cha Algeria baada ya kuteuliwa kwenye kikosi cha wachezaji 18 kwa ajili ya mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Nigeria Uwanja wa Kimataifa wa Akwa Ibom, Novemba 12.
  Kikosi hicho chenye wachezaji 17 wanaocheza nje, kitaongozwa na wachezaji wawili wa klabu bingwa y England, Leicester City, Riyad Mahrez na Islam Slimani, wakati Nabil Bentaleb wa Schalke 04 ya Ujerumani pia ameorodheshwa.
  Nyota wa West Ham United, Sofiane Feghouli, Yacine Brahimi, Ryad Boudebouz na Mehdi Abeid ni miongoni mwa walioitwa. Kinda Adam Ounas hatimaye amebadilisha uraia kutoka Mfaransa hadi Mualgeria na ameitwa kikosini safari hii.
  Rais M’Bolhi (katikati) waliosimama ndiye kipa pekee aliyeitwa kwa ajili ya mechi na Nigeria

  Rais M’Bolhi wa Antalyaspor ni kipa pekee aliyeitwa kwa ajili ya mchezo huo.
  Nigeria inaongoza Kundi B la Kanda ya Afrika Africa kuwania tiketi ya Kombe la Dunia mwaka 2018 Urusi ikiwa na pointi tatu baada ya kuifunga Zambia 2-1 mjini Ndola mwezi uliopita, wakati Algeria iligawana pointi na Cameroon kwa sare ya 1- katika mechi yao ya kwanza ya kundi hilo.
  Kikosi kamili cha Algeria kilichoitwa kwa ajili ya Nigeria ni kipa; Rais M’Bolhi (Antalyaspor, Uturuki), manbeki; Carl Medjani (CD Leganés, Hispania), Liassine Cadamuro (Servette Geneva, Uswisi), Hicham Belkaroui (ES Tunis), Aissa Mandi (Real Betis, Hispania) na Faouzi Ghoulam (Napoli, Italia).
  Viungo; Yacine Brahimi (FC Porto Ureno), Sofiane Feghouli (West Ham United, England), Nabil Betaleb (Schalke 04, Ujerumani), Rachid Ghezzal (Olympique Lyon, Ufaransa), Mehdi Abeid (Dijon FCO, Ufaransa), Adlène Guedioura (Watford FC, England), Sapphire Taïder (Bologna FC, Italia), Ryad Boudebouz (Montpellier Hérault, Ufaransa) na Adam Ounas (Bordeaux, Ufaransa).
  Washambuliaji ni: Hilal Soudani El Arabi (Dinamo Zagreb, Croatia), Riyad Mahrez (Leicester City, England), Islam Slimani (Leicester City, England).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ALGERIA YAITA KIPA MMOJA KUIVAA NIGERIA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top