• HABARI MPYA

  Saturday, October 15, 2016

  YANGA YAZIFUNIKA AZAM NA SIMBA VIWANGO VYA CAF

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa viwango vya ubora wa klabu barani, huku Yanga ikiongoza kwa klabu za Tanzania.
  Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Yanga SC imeshika nafasi ya 331 mbele ya Azam FC iliyo katika nafasi ya 351, wakati klabu nyingine ya Tanzania iliyoingia ni Simba SC iliyo katika nafasi ya 356.
  Esperance ndiyo inaongoza kwa ubora wa soka Afrika, ikifuatiwa na Etoile du Sahel, zote za Tunisia, TP Mazembe, AS Vita zote za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), El Merreikh ya Sudan, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Al Ahly ya Misri, Al Hilal ya Sudan, Zamalek ya Misri na Coton Sport ya Cameroon katika 10 Bora.
  Wazi mafanikiko ya Yanga kufika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika mwaka huu yatakuwa yameibeba mwaka huu kuwazidi wapinzani, Azam na Simba.
  Yanga ilishika mkia katika Kundi A Kombe la Shirikisho, ambalo TP Mazembe na MO Bejaia zilifuzu Nusu Fainali na baadaye Fainali baada ya kuzitoa timu za Kundi B.
  Ikumbukwe Yanga SC iliyoshinda mechi moja dhidi ya Bejaia 1-0 na kutoa sare moja dhidi ya Medeama ya Ghana mechi zote za Dar es Salaam, ilifuzu hatua ya makundi baada ya kuitoa Sagrada Esperanca ya Angola katika mchezo maalum wa mchujo.
  Na Yanga iliangukia kwenye kapu la kuwania hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho baada ya kutolewa na Al Ahly ya Misri katika hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAZIFUNIKA AZAM NA SIMBA VIWANGO VYA CAF Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top