• HABARI MPYA

    Sunday, October 09, 2016

    YANGA WAITISHA MKUTANO WA DHARULA TENA OKTOBA 23

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    UONGOZI wa Yanga umeitisha mkutano wa dharula wa wanachama wote utakaofanyika Jumapili ya Oktoba 23, mwaka huu katika ukumbi ambao utatajwa baadaye.
    Taarifa ya Kaimu Katibu wa Yanga, Baraka Deusdedit imesema kwamba wanachama wote wanatakiwa kufika bila kukosa kwa sababu mkutano huo ni kwa faida na maslahi mapana ya klabu.
    Deusdedit alisema agenda za mkutano pamoja na mahali utakapofanyika vitatajwa baadaye.
    Mwenyekiti wa Yanga, Yussuf Manji atakuwa mmiliki wa klabu kwa miaka 10 ijayo

    Mkutano huo unafuatia Baraza la Wadhamini la Yanga SC kuikodisha timu ya soka kwa kampuni ya Yanga Yetu, inayomilikiwa na Mwenyekiti wa klabu, Yussuf Manji ambayo itakuwa mmiliki wa klabu kwa miaka 10 ijayo.
    Na hatua ya Baraza ilifuatia azimio la wanachama wa klabu hiyo Agosti 6, katika Mkutano wa dharula pia kukubali kumkodisha klabu hiyo kiongozi wao huyo mkuu kwa miaka 10.
    Manji aliomba apewe klabu kwa miaka 10 na katika kipindi hicho atakuwa anachukua asilimia 75 ya mapato ya timu, huku asilimia 25 ikibaki kwa wanachama.
    Na katika kipindi hicho cha miaka 10, timu ya soka na nembo ya klabu zote zitakuwa chini yake Manji. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA WAITISHA MKUTANO WA DHARULA TENA OKTOBA 23 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top